Home Kimataifa MADRID YATOA DOZI NENE LA LIGA, BBC YAHUSIKA

MADRID YATOA DOZI NENE LA LIGA, BBC YAHUSIKA

584
0
SHARE

BBC

Real Madrid imeisulubu Getafe kwa bao 5-1 kwenye mchezo wa La Liga na kuanza kuwapumulia mgongoni vinara wa ligi hiyo Barcelona.

Karim Benzema alianza kufungua gharika hiyo kwa kumalizia krosi iliyochongwa na James Rodriguez.

Isco akaongeza bao la pili kabla ya kwenda mapumziko akitumia vema pande la Benzema.

Gareth Bale aliongeza bao la tatu dakika tano tangu kuanza kwa kipindi cha pili baada ya kukimbia na mpira kabla ya kuujaza wauni, kwa mara nyingine shukrani kwa pasi ya mwisho kutoka kwa Benzema.

Dakika ya 83 Getafe walipata bao kupitia kwa mshambuliaji Pablo Sarabia lakini bado halikutosha kuwapunguza kasi vijana wa Zizou kwani James Rodriguez aliongeza bao linguine la nne.

Cristiano Ronaldo akamaliza shughuli kwa kufunga bao rahisi na kukamilisha idadi ya magoli matano huku washabuliaji watatu wa timu hiyo Benzema, Bale na Cristiano (BBC) wote wakiwa wametumbukia kambani.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here