Home Ligi BUNDESLIGA Fainali ya UCL baina ya City vs Bayern – Huenda ikamfanya Pep...

Fainali ya UCL baina ya City vs Bayern – Huenda ikamfanya Pep Guardiola Ajiuzulu

620
0
SHARE

Pep Guardiola amefanikiwa kuwakwepa wachezaji wake wa waajiri wake wajao Manchester City wakati Bayern Munich ilipopangwa kucheza dhidi ya Atletico Madrid katika nusu fainali ya Champions League.

 Lakini kuwakwepa sasa inawezekana ni kuchelewesha tu mkutano wao, bado kuna uwezekano kocha huyo akakutana na City fainali na kukawepo na mgongano wa kimaslahi

Ikitokea City na Bayern Munich wakakutana kwenye fainali ya tarehe 28 mwezi ujao, Guardiola atakuwa mpinzani wa waajiri wake wapya katika kugombea ubingwa mkubwa zaidi katika historia ya Manchester City.

 Ikitokea City wakaikosa nafasi ya 4 katika Premiwr League – kwa aidha West Ham au Manchester United – basi Guardiola
sio tu atakuwa katikati ya ndoto za matajiri wa City kutwaa UCL bali pia kujipa wakati mgumu msimu ujao kwa kutoshiriki UCL, kutokana na haya kuna uwezekano akawa kwenye presha kubwa ya kujiuzulu kuifundisha Bayern Munich kabla ya mchezo wa fainali.

Guardiola ataingia kwenye mechi hiyo akijua kwamba ushindi utamaanisha kwamba hatoshiriki kwenye michuano hiyo msimu ujao, wakati akijua kipigo kwa Bayern kitamaanisha kwamba City watakuwemo msimu ujao kuutetea ubingwa wao.
Kwa hakika Guardiola atakuwa kwenye wakati mgumu na sijui kwa namna gani nyingine ataondoka kwenye mgongano huo, hata kama hakuna shaka anataka kuondoka Bayern akiacha legacy kubwa kwa kutwaa kombe hili.

Anaweza kuingia kwenye mchezo huo na kwa bahati mbaya mbinu zake zikazidiwa na kocha mwenzie na kupoteza bahati mbaya, kwa hakika maneno yatakuwa mengi.

 Kwa sasa Guardiola ana mengi ya kufikiria mbele ya kukutana na Atletico ambao ni kiukweli ni mlima mrefu kuupanda. Lakini ama kwa hakika Guardiola atakuwa anaziombea mabaya sana West Ham na Manchester United ili mambo yakae sawa ikitokea City na Bayern wamekutana fainali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here