Home Kitaifa BAADA YA KIMYA KIREFU, HANS POPPE AMEAMUA KUTOA YA MOYONI KUHUSU SAKATA...

BAADA YA KIMYA KIREFU, HANS POPPE AMEAMUA KUTOA YA MOYONI KUHUSU SAKATA LA RUSHWA NA UPANGAJI MATOKEO

687
0
SHARE

Hans-Poppe

Sakata la rushwa na upangaji matokeo ambapo viongozi kadhaa wa TFF wakiwa ni watuhumiwa, bado wadau wa soka nchini wameendelea kutoa maoni yao kuhusu kashfa hiyo nzito inayolikabili soka la Bongo huku wakielezea pia nini kifanyike.

Mwandishi wa habari za michezo kutoka Clouds Media Group Yahaya Mohamed amefanya mahojiano na Mjumbe wa kamati ya Utendaji ya Simba SC  na Mwenyekiti wa kamati ya usajili ya klabu hiyo Zacharia Hans Poppe ambaye ametoa maoni yake kuhusu ‘zengwe’ hilo huku akisema wahusika wamechelewa kujiuzulu kutokana na tuhuma zinazowakabili.

Nakuunganisha na Yahaya Mohamed ili ujue mpango mzima uliendaje na Hans alifunguka yapi katika mahojiano hayo, endelea…

Yahaya: Hivi karibuni zimenaswa sauti za maafisa wa TFF wakipanga mipango ya kuomba rushwa ili kuzisaidia timu fulani, unazungumziaje masuala ya rushwa katika mchezo wa soka?

Hans Poppe: Hili suala hata mimi nimewahi kulizungumzia huko nyuma, ni kweli haya mambo yanatokea ni kiasi cha kuyatafutia ushahidi lakini mara nyingine ushahidi unapata kwenye mazungumzo ya watu wenyewe. Kupanga matokeo maana yake unazungumza na waamuzi au wachezaji waachie mchezo na vitu kama hivyo.

Hii ‘clip’ iliyopatikana ya wale watu  wa TFF wanafanya mambo kama hayo, sasa mambo ya namna hii ukianza kuyaangalia tokea mwanzo utakuta hilo suala lipo, unachotakiwa kufanya ni kulitafutia ushahidi.

Sasa kama limetokea kwa viongozi na ikapatikana clip kuna mambo mengine mengi kwasababu hii clip ni watu wameweza kurekodi lakini bado hawa watu wanaweza wakazungumza kwa mdomo kwamba sisi tuliambiwa vitu fulani, ule ni ushahidi wa moja kwa moja mtu anasema kwamba, mimi niliambiwa na kiongozi fulani nifanye hivyo ili timu fulani ishinde. Huko kote ni kupanga matokeo.

Athari kubwa za kupanga matokeo kutafuta timu fulani iwe bingwa, inakuja kutukuta kwenye international matches. Ukitazama kiwango chetu kwenye mechi za kimataifa kwa miaka kadhaa iliyopita ni kibovu kwasababu bingwa anayepatikana kwenye ligi ya kwetu anakuwa bingwa anayekwenda kwa mbinu za namna hiyo. Inatia aibu nchi, inaharibu mpira wetu, mimi naweza kusema wazi nikitazama uongozi mpya wa TFF ni mbaya sana.

Kama hatuwezi kufanya mabadiliko yeyote au maamuzi magumu ya kubadilisha mfumo mzima hakuna namna ambayo mpira wetu unaweza kuendelea, utazidi kudumaa.

Yahaya: Tumesikia wadhamini wa ligi kuu (Vodacom) wamesema wanafanya uchunguzi juu ya sakata hili na huenda wakajitoa kama ikithibitika hivyo, unazungumziaje hili?

Hans Poppe: Ni kweli kwasababu hawawezi kujihusisha na mambo kama hayo unavyowekeza pesa yako unategemea unasaidia jambo halafu baadaye badala ya kuwa unasaidia unasikia linaharibiwa na mambo kama hayo, uendelee kusaidia kwasababu gani?

Mimi ninaamini Vodacom wanapotoa mchango wao kuidhamini ligi wanakuwa wanachangia kwenye jamii wanategemea kupata faida fulani, mimi naunga mkono kabisa kama kweli haya masuala yanafanyika na Vodacom wakichunguza wakikuta yanafanyika waondoke tu.

Watafute wadhamini wanaojihusisha na madawa ya kulevya, wauza pembe za ndovu ndiyo wafadhili vitu kama hivyo kwasababu haramu siku zote huzaa haramu. Huwezi kuwa na kitu chako cha halali ukaenda kuchangia kitu haramu.

Yahaya: Kwa sakata hili unadhani huu ni muda mwafaka kwa viongozi wa TFF kujiuzulu?

Hans Poppe: Tena nafikiri umepita, kunamatukio mengi ambayo sisi tumeyasemea kwamba kwa uongozi huu unaoendelea sasahivi na mambo wanayoyafanya hawastahili kuwepo pale.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here