Home Dauda TV TOTTENHAM YAVUNJA UTAWALA WA MAN UNITED WHITE HART LANE (Video)

TOTTENHAM YAVUNJA UTAWALA WA MAN UNITED WHITE HART LANE (Video)

690
0
SHARE

Spurs vs Man United

Tottenham wameendelea kuifukuzia ndoo ya Premier League baada ya kuibuka na ushindi mzito dhidi ya Manchester United.

Kufatia Leicester kutoa kichapo kwa Sunderland mapema leo, Tottenham imepiga goli tatu ndani ya dakika sita na kukaa nafasi ya pili kwa tofauti ya ponti saba dhidi ya vinara Leicester.

Dele Alli alianza kuzifungua nyavu za United baadadae Toby Alderweireld akapachika bao la pili kwa kicha kabla ya Erik Lamela kumaliza shughuli kwa kupasia kamba ya tatu na kuumaliza mchezo.

Mchezo huo ulichelewa kuanza kwa nusu saa kufatia basi la timu ya Manchester United kukwama kwenye mataa ya London wakati wakielekea kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Takwimu muhimu:

  • Spurs ilikuwa haijashinda dhidi ya United kwenye uwanja wao wa nyumbani tangu mwaka 2001, michezo 14 ilishapita wakati kocha Mauricio Pochettino alikuwa hajashinda michezo sita iliyopita dhidi ya United.
  • Manchester United imeshindwa kupiga shuti hata moja lililolenga lango la Tottenham kwenye vipindi vya kwanza vya mechi za ligi msimu huu.
  • Dele Alli amefunga goli la kwanza kwenye uwanja wa White Hart Lane tangu alipofanya hivyo mwezi November alifunga goli dhidi ya Aston Villa
  • Tofauti ya goli la kwanza la Spurs na goli la tatu ilikuwa ni dakika tano na sekunde 46

Video ya magoli yote Tottenheam 3-0 Manchester United

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here