Home Kimataifa PACQUIAO ALIPA KISASI, AMCHAPA MMAREKANI NA KUTUNDIKA GLOVES

PACQUIAO ALIPA KISASI, AMCHAPA MMAREKANI NA KUTUNDIKA GLOVES

629
0
SHARE

Pacquiao

Manny Pacquiao amemchapa Timothy Bradley kwa ushindi wa majaji wote kwenye pambano ambalo mfilipino huyo amesema ni la mwisho kwenye maisha yake ya masumbwi.

Majaji wote watatu wamempa ushindi Pacquiao wa ponti 116-110 kwenye pambano lililofanyika kwenyika Las Vegas, Marekani.

“Nimeshakubaliana na familia yangu kwamba, baada ya pambano hili nastaafu”, amesema Pacquiao.

Pacquiao ameibuka na ushindi huo wa pont ikiwa ni kisasi baada ya kuchezea kichapo kutoka kwa Bradley mwaka 2009 kwenye pambano lao la kwanza, Pacquiao alishinda pambano la marudiano mwaka 2014 kabla ya kushinda tena kwenye pambano lililowakutanisha kwa mara ya tatu.

Bradley alilambishwa sakafu mara mbili kwenye pambano hilo, roundi ya saba bondia huyo wa Marekani aligalagazwa chini baada ya kupewa ‘bomba’ ya kabla ya kurudishwa tena chini raundi ya tisa.

“Ninafurahia kuwa mstaafu, nataka nihudumie na kuwasaidia watu”, aliongeza Pacquiao, ambaye anasema anataka kuwekeza muda mwingi kwenye mambo yake ya kisiasa huko Ufilipino.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here