Home Dauda TV ORIGI AMEANZA KUELEWEKA LIVERPOOL

ORIGI AMEANZA KUELEWEKA LIVERPOOL

628
0
SHARE

Origi

Divock Origi ametupia kambani bao mbili akitokea benchi kwenye mchezo wa Premier League ambao Liverpool imepata ushindi wa magoli 4-1 dhidi ya Stoke na kupanda kwa nafasi moja hadi nafasi ya tisa kwenye msimamo wa ligi.

Shuti la Alberto Moreno liliipa Liverpool bao la kuongoza kabla ya Bojan hajachomoa bao hilo.

Daniel Sturridge aliunganisha krosi ya Sheyi Ojo na kuiweka Liverpool mbele kwa mara nyingine tena kisha Origi akafunga magoli mawili baadaye.

Klopp alimchezesha Origi kama mshambuliaji pekee kwenye mchezo wa kwanza war obo fainali dhidi ya Borussia Dortmund lakini Sturridge alianza kwenye mchezo dhidi ya Stoke City na kuonekana yuko fit.

Baada ya Moreno kupiga bao la kwanza, mshambuliaji huyo wa England alipiga bao la pili akimalizia krosi ya Ojo.

Orig pia alionesha makali yake akiongeza nguvu upande wa safu ya uhambuliaji ya Liverpool baada ya kuingia kipindi cha pili akitokea benchi. Mbeligiji huyo angepiga hat-trick kama angeunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Moreno.

Sturridge na Orig walishirikiana vizuri huku Sturridge akifanikiwa kucheza kwa dakika zote 90 kwa mara ya kwanza tangu February 28.

Video ya magoli yote Liverpool 4-0 Stoke City

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here