Home Kimataifa MESSI AMECHEZA SAA 6 BILA KUONA NYAVU

MESSI AMECHEZA SAA 6 BILA KUONA NYAVU

692
0
SHARE

Messi-disapointed

Juma lililopita Barcelona ilichapwa bao 2-1 na Real Madrid kwenye uwanja wao wa nyumbani kwenye mechi ya El Clasico, Jumamosi usiku kikosi cha Luis Enrique kimepoteza tena mchezo wa ligi kikiwa ugenini dhidi ya Real Sociedad.

Mikel Oiarzabal gave the hosts the lead in the fifth minute, and Barca couldn’t find a way back into the game.

Mikel Oiarzabal aliifungia Sociedad bao pekee dakika ya 5 kipindi cha kwanza lililowapa pointi tatu huku Barca ikishindwa kusawazisha goli hilo hadi dakika 90 zinamalizika.

Kichapo hicho kimewafanya Barca kusogelewa na Atletico Madrid kwenye mbio za ubingwa ambapo sasa Barcelona inaididi Atletico kwa pointi tatu, Barcelona ambao ndiyo vinara wa ligi wanapointi 76 wakifuatiwa na Atletico yenye pointi 73 huku Madrid ikiwa nyuma yao na pointi zake 72 wakati huo timu zote zikiwa zimecheza mechi 32 na kusaliwa na mechi sita pekee ili msimu kumalizika.

Kiwango cha star wa Barcelona Leo Messi kinalalamikiwa kushuka kwa kaiasi kikubwa tangu alipokuwa kwenye kiwango kibovu kama hicho mwaka 2011.

May 2011 ilikuwa ni mara ya mwisho kwa Leo Messi kucheza mechi nne mfululizo akiwa Barca bila kufunga wala kutoa assist.

Messi-2011

Sasa zimeshapita saa sita (dakika 362) tangu Messi afunge bao lake la mwisho au kutoa assist akiwa ametinga uzi wa Barcelona.

Messi alipiga mashuti saba kwenye mchezo dhidi ya Sociedad, lakini bado hayakusaidia chochote huku ikiwa ni idadi kubwa ya mashuti aliyopiga kwenye mchezo wa La Liga msimu huu.

Messi bado yuko nafasi ya tatu kwenye orodha ya wafungaji akiwa ameshatupia nyavuni mara 22 huku ronaldo ikiongoza orodha ya wafungaji akiwa na mabao 30.

Kwenye orodha ya wachezaji waliotoa assist nyingi, Messi anaungana na Gareth Bale pamoja na Koke wote wakiwa na assist 10 wakati Ronaldo na Neymar wakiwa na assist 11 huku Luis Suarez akiwa ndiye king wa assist baada ya kufanya hivyo mara 13.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here