Home Dauda TV KWANINI VARDY ALIPIGA BAO MBILI DHIDI YA SUNDERLAND? RANIERI AMETOA MAJIBU (Video)

KWANINI VARDY ALIPIGA BAO MBILI DHIDI YA SUNDERLAND? RANIERI AMETOA MAJIBU (Video)

639
0
SHARE

Vardy-Ranieri 1

Striker wa Leicester City Jamie Vardy anafanya kila linalowezekana ili ajihakikishie nafasi katika kikosi cha kwanza cha England kitakachocheza michuano ya Euro majira ya joto mwaka huu nchini Ufaransa.

Mshambuliani huyo mwenye miaka 29 ameifungia timu yake magoli mawili na kuukaribia ubingwa wa Premier League pale timu yake ilipoizamisha Sunderland kwa magoli 2-0.

Akizungumza baada ya mechi, kocha wa Leicester Claudio Ranieri amewaambia wandishi wa habari kwamba, alichomwambia Jamie Vardy wakati wa mapumziko kiliamsha hamasa na kupelekea kufunga.

“Nimefurahi sana kwasababu wiki iliyopita hakufunga japo alitoa assist kwa Mahrez ambaye alifunga goli. Lakini leo wakati wa mapumziko nilimwambia Jamie nataka ufunge”, amesema manager huyo raia wa Italia.

Video: Ranieri akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo Sunderland vs Leicester 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here