Home Dauda TV ‘KIDUKU’ CHAKO PELEKA HUKO, SAUDI ARABIA WANANYOLEWA UWANJANI (Video)

‘KIDUKU’ CHAKO PELEKA HUKO, SAUDI ARABIA WANANYOLEWA UWANJANI (Video)

842
0
SHARE

Saudi Arabis

Tukio la kushangaza kwenye mchezo wa soka limetokea nchinin Saudi Arabia weekend hii pale ambapo mechi ilisimamishwa kwa ajili ya kupicha golikipa anyolewe nywele zake ambazo zilikuwa ni kinyume na maadili ya dini ya Kiislam.

Haijafahamika haraka jina la golikipa huyo wala timu ambazo zilikuwa zinacheza mchezo huo, lakini picha za video inaonesha tukio zima la golikipa huyo akinyolewa.

Mchezo ulisimama na ofisa mmoja akafuata golikipa huyo kwa ajili ya kuzikata nywele zake uwanjani, haikujulikana moja kwa moja ni nywele zipi ambazo zilikuwa kinyume na maadili.

Golikipa huyo aliambiwa achugue mambo mawili; kuacha kucheza na kutoka nje ya uwanja au kunyolewa, akaamua kukubali kunyolewa nywele zake.

Kwa mujibu wa taarifa, tukio hilo limekuja ikiwa ni agizo kutoka kwa mamlaka za Saudi Arabia ambazo zimeamua kuchukua hatua dhidi ya style za unyoaji wa nywele ambazo ni kinyume na uislam.

Angalia huyu golikipa anavyonyolewa huku mchezo ukiwa umesimama kupisha zoezi hilo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here