Home Kimataifa CRISTIANO RONALDO AANDIKA REKODI MPYA LA LIGA

CRISTIANO RONALDO AANDIKA REKODI MPYA LA LIGA

677
0
SHARE

Ronaldo-Rekodi

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 30 ndani ya misimu sita ya La Liga baada ya Madrid kuichapa Eibar kwa bao 4-0 kwenye mchezo wa ligi.

Karim Benema ambaye anapambana na majeruhi ya goti pamoja na Gareth Bale walipumzishwa wakati Madrid inasubiri mchezo wa marudiano siku ya Jumanne wa klabu bingwa Ulaya dhidi ya Wolfsburg.

James Rodriguez alianza kuzifungua nyavu za Eibar kwa mkwaju wa mpira wa adhabu ndogo kabla ya Lucas Vazquez hajapachika bao la pili.

Hadi mapumziko tayari Madrid ilikuwa mbele kwa magoli 4-0 huku Ronaldo akitumbukia nyavuni kupiga bao la tatu akiunganisha pasi ya Jese ambaye naye alipiga bao na kukamisha idadi ya magoli 4-0.

Real inakumbuka kichapo cha magoli 2-0 kutoka kwa Wolfsburg wakati ikijiandaa na mchezo wao wa marudiano kwenye uwanja wa Bernabeu huku kocha wa klabu hiyo Zinedine Zidane kiweka wazi kwamba, endapo watashindwa kufuzu kwa hatua ya nusu fainali basi msimu wao utakuwa umemaliza.

Kikosi cha Zidane kwa sasa kipo nyuma ya vinara wa ligi hiyo (Barca) kwa pointi nne nyuma kikisimama nafasi ya tatu nyuma ya Atletico Madrid.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here