Home Dauda TV BUFFON KWENYE UBORA WAKE AINYIMA USHINDI AC MILAN (Video)

BUFFON KWENYE UBORA WAKE AINYIMA USHINDI AC MILAN (Video)

519
0
SHARE

Buffon

Kwa namna mambo yanavyokwenda kwa miaka ya hivi karibuni, si jambo la kushangaza Juventus kuitungua AC Milan kwa bao 2-1 kwenye uwanja wa San Siro.

Kabla ya game hiyo kupigwa, kulikuwa na utoaji wa heshima kwa Cesare Maldini nahodha na kocha wa zamani wa Rossoneri na baba wa mlinzi wa zamani wa AC Milan Paolo ambaye alifariki mwishoni mwa juma lililopita.

AC Milan ambao wako nafasi ya sita kwenye msimamo wa Serie A kwa sasa, walitangulia kupata bao dakika ya 18 kupitia kwa Alex lakini magoli ya Mario Mandzukic na Paul Pogba yaliipa ushindi Juve.

Buffon ameendelea kuwa katika kiwango bora baada ya kushuhudia akifanya saves za kutosha kwenye mchezo dhidi ya AC Milan na kuiweka salama timu yake iliyoibuka na ponti tatu ugenini.

Ushindi huo umeipeleka Juventus pointi tisa juu ya Napoli ambao wako nafasi ya pili huku Juve wakionekana wazi kulitwaa taji la Seriea A kwa mara nyingine tena.

AC Milan walipata nafasi kadhaa za kufunga lakini kiwango cha Gianluigi Buffon kilikuwa mwiba kwao kutokana na mkongwe huyo kuwanyima kabisa nafasi ya kupasia kamba.

Mzee huyo wa miaka 38 inawezekana kwa sasa yuko kwenye kiwango cha juu kuwahi kutokea kwenye maisha yake ya soka.

Angalia mambo aliyoyafanya Buffon kwenye mchezo wa AC Milan vs Juventus 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here