Home Kimataifa AZAM YAKOMAA MBELE YA WAARABU CHAMAZI

AZAM YAKOMAA MBELE YA WAARABU CHAMAZI

715
0
SHARE

Kipre 2

Azam imeutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani Azam Complex, Chamazi baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa raundi  ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Esperance ya Tunisia.

Esperance ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza lilifungwa na Heithem Jouini dakika ya 34 kipindi cha kwanza na kudumu kwa dakika zote 45 za kwanza.

Kipre 1

Kipindi cha pili Azam ilifanya mabadiliko ya mapema kwa kumtoa Michael Balou na nafasi yake kuchukuliwa na Frank Domayo mabadiliko yaliyoleta tija kwa kuzaa bao la kusawazisha lililofungwa na Farid Musan dakika ya 68.

Azam ilifanya mabadiliko mengine kwa kumpumzisha Waziri Salum na kumuingiza Khamisi Mcha ambapo kasi ya Azam iliongezeka zaidi na kufanikiwa kuzaa bao la pili dakika ya 70 kupitia kwa Ramadhani Singano ‘Messi’ ambaye alikuwa kwenye kiwango bora kwenye mchezo wa dhidi ya Esperance.

Kipre

Kikosi cha Stewart Hall kitajilaumu kwa kupoteza nafasi nyingi za kufunga na kutoka na ushindi mkubwa lakini washambuliaji wake walikosa umakini na utulivu kila mara walipofika langoni.

Takwimu muhimu za kufahamu:

  • Azam haijapotea mchezo wa kimataifa ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani (Azam Complex) tangu ilipoanza kuutumia uwanja huo kwa mechi za kimataifa.
  • Azam imekutana na Esperance kwa mara ya kwanza kwenye michuano ya Afrika tangu ilipoanza kucheza mashindano hayo.
  • Timu zote mbili (Azam na Esperance zimetinga raundi ya pili kwa kuwatoa wapinzani wao kwa wastani wa magoli saba. Azam FC ikiitoa Bidvest Wits ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 7-3 huku Esperance nayo ikiifurusha nje Renaissance ya Chad kwa ushindi wa 7-0.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here