Home Kitaifa YANGA YABANWA TAIFA, MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA MISRI

YANGA YABANWA TAIFA, MBIVU NA MBICHI KUJULIKANA MISRI

898
0
SHARE
Mchezaji wa Yanga Issoufou Boubacar akiwa chini huku wachezaji wa Al Ahly wakiondosha mpira kwenye eneo lao la hatari

Klabu ya Yanga imeshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kulazimishwa sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Al Ahly ya Misri kwenye mchezo wa klabu bingwa Afrika uliopigwa kwenye uwanja wa taifa.

Al Ahly walikuwa wakwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 9 kipindi cha kwanza mfungaji akiwa ni Amri Gamal ambaye aliukwamisha wavuni mpira wa adhabu ndogo ambao haukuokolewa na mabeki wa Yanga.

Golikipa wa Al Ahly akiwa ameuweka mpira kwenye himaya yake
Golikipa wa Al Ahly akiwa ameuweka mpira kwenye himaya yake

Dakika ya 19 Yanga walipata bao la kusawazisha baada ya beki wa Al Ahly kujifunga wakati akijaribu kuokoa krosi iliyopigwa na winga wa kimataifa wa Niger Issoufou Boubacar na kuipa Yanga goli la kusawazisha.

Timu hizo zilikwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana bao 1-1 matokeo ambayo yalidumu kwa dakika zote za mchezo.

Yanga watasafiri kwenda Misri kwa ajili ya kucheza mchezo wa marudiano ambao utachezwa kati ya April 19 au 20. Mchezo huo ndiyo utaamua timu ipi itakayosonga mbele ya mashindano.

Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akichuana na baeki wa Al Ahly Rami Rabea
Mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma akichuana na baeki wa Al Ahly Rami Rabea wakati wa mchezo wa klabu bingwa Afrika uliochezwa uwanja wa taifa

Kivutio kikubwa kwenye mechi hiyo ilikuwa ni mashabiki wa Al Ahly ambao walikuwa wakiimba na kupiga ngoma kuishangilia timu yao kwa dakika zote za mchezo kitu ambacho mashabiki wa kibongo wanatakiwa kujifunza.

Mashabiki wa Al Ahly ya Misri wameuteka uwanja wa taifa wakii-support timu yao
Mashabiki wa Al Ahly ya Misri wameuteka uwanja wa taifa wakii-support timu yao

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here