Home Kitaifa WALIOKATA TAMAA KUHUSU YANGA KUSONGA MBELE MICHUANO YA AFRIKA, HILI NI NENO...

WALIOKATA TAMAA KUHUSU YANGA KUSONGA MBELE MICHUANO YA AFRIKA, HILI NI NENO LA VAN PLUIJM KWENU

761
0
SHARE
Hans van Pluijm-Kocha mkuu wa Yanga SC
Hans van Pluijm-Kocha mkuu wa Yanga SC
Hans van Pluijm-Kocha mkuu wa Yanga SC

Kocha wa Yanga Hans van Pluijm amesema bado anaimani kubwa ya kusonga mbele kwenye michuano ya klabu bingwa Afrika licha ya kikosi chake kushindwa kuibuka na ushindi mbele ya Al Ahly wakiwa kwenye uwanja wa nyumani.

Pluijm ansema kwenye soka chochote kinaweza kutokea na kuwa na matumaini ni jambo zuri, lakini hakuacha kusema kwamba matokeo waliyopata kwenye uwanja wao wa nyumbani siyo mazuri kwasababu walitakiwa kushinda wakiwa nyumbani.

“Ni mara ya tano sasa nakutana na Al Ahly nafahamu wanauwezo wa kupasiana na kuuteka mchezo, tulianza vizuri na tulitaka kuwa wa kwanza kupata goli lakini timu za Misri zinajua kufanya mashambulizi ya kushtukiza, hatukuwa makini wakati mpira wa adhabu ndogo unapigwa”, anasema kocha wa Yanga ambaye timu yake itahitaji ushindi wa aina yoyote ili kufuzu moja kwa moja kwa hatua inayofuata.

“Baada ya hapo vijana walipambana na ninawapongeza kwasababu tulisawazisha bao japo sare si matokeo mazuri unapokuwa kwenye uwanja wa nyumbani, lakini kwa ujumla tumecheza vizuri”.

“Kweli walitawala mchezo kwa kipindi cha pili na hiyo inatokna na baadhi ya wachezaji wao kucheza pamoja kwa zaidi ya miaka sita na hiyo ni faida kwao”.

“It is not over until it is over, unatakiwa kuwa na matumaini kwenye mchezo wa soka kilakitu kinawezekana, nafasi ya Yanga kufuzu bado ipo”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here