Home Dauda TV SAMATTA AONESHA THAMANI YA NAMBA 77 (Video)

SAMATTA AONESHA THAMANI YA NAMBA 77 (Video)

826
0
SHARE

Samatta 77

Mbwana Samatta ameendelea kufanya vyema akiwa na klabu ya Genk baada ya kutupia kambani bao moja wakati timu yake ikiiua Oostende kwa magoli 4-0.

Samatta aliingia uwanjani dakika ya 77 kisha kupachika bao ndani y dakika ya 77 akiwa ametika jezi yenye namba 77 mgongoni.

Kabla ya Samatta kuingia uwanjani kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis, Genk ilikuwa mbele kwa magoli 2-0 lakini mara baada ya kutinga tu uwanjani alipachika bao hilo na kuifanya timu yake kuwa mbele kwa magoli 3-0.

Magoli mengine ya Genk yamepachikwa wavuni na Puzuelo, Buffel pamoja na Kebano.

Samatta sasa amefikisha jumla ya magoli matatu tangu ajiunge na timu ya Genk huku akifanikiwa kuthibitisha kuwa yeye ni striker wa kimataifa kwa kufunga magoli hayo akiwa ametumia miguu yote pamoja na kichwa.

  • Bao la kwanza akiwa Genk alilifunga kwa mguu wa kuli
  • Akafunga bao lake la pili kwa kichwa
  • Kisha bao lake la tatu amelifunga kwa mguu wa kushoto.

Angalia video ya bao la Samatta alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Oostende

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here