Home Ligi EPL Mourinho azungumzia ajira mpya – viashiria vinaonyesha Old Trafford ndio kituo kipya...

Mourinho azungumzia ajira mpya – viashiria vinaonyesha Old Trafford ndio kituo kipya cha ajira.

793
0
SHARE

Huku tetesi za kujiunga kwake na Manchester United zikiwa zimeshika hatamu, leo kocha wa kireno Jose Mourinho amefanya mahojiano yaliyochapishwa na gazeti la Ureno O Jogo.  

 Kocha huyo wa zamani wa Chelsea na Real Madrid amesisitiza anatarajia kufundisha wakati wa kiangazi lakini hana uhakika atafundisha timu gani. 

Jose Mourinho amekaririwa akisema kwamba ana ofa kadhaa mezani lakini anataka kwenda sehemu ambayo anahitajika kiukweli.  

 “Ninakuhakikishia kwamba nitarejea kazini wakati wa kiangazi. Nina ofa nzuri mezani. 

“Ni jambo la kufikiria, kisha kufanya maamuzi sahihi na kusaini mkataba. Wakati wa kiangazi, mwishoni mwa msimu, kila mtu atafahamu klabu yangu mpya.” 

“Kitu cha uhakika, sitkuwa kocha wa Estoril au Paços, kwa sababu wote wana misimu mizuri na hawawezi kubadili kocha.”  
“Nitapeleka ujuzi wangu sehemu ambayo nahitajika kwa dhati. Nataka niende sehemu ambayo natakiwa niwepo kiukweli.”  
“Nataka kufanya kazi katika klabu ambayo ina majukumu mazito, kwenye ligi ngumu, ambapo hakuna malengo mepesi. Hayo yananifanya nisiwe na machaguo mengi.” 

  
Sentensi hii ya mwisho inaonyesha kwa kiasi fulani kwamba Mourinho anaelekea England kwenye ligi yenye ushindani mgumu – klabu yenye majukumu mazito ambayo kwa sasa inayumba ni Manchester United. Klabu nyingine ya ligi nyingine ngumu yenye sifa alizotaja ni Real Madrid. 

Wachambuzi wengi wa michezo barani wanaamini Mourinho ataenda Old Trafford na tangazo lake la ajira litatolewa mwishoni mwa msimu au pale itakapothibitika kimahesabu kwamba United haitoweza kumaliza katika nafasi 4 za juu za kufuzu ulaya – Van Gaal atakutana na barua ya kuvunjiwa mkataba na Mourinho atatangazwa kumrithi kuanzia msimu ujao.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here