Home Kimataifa KOCHA WA AL AHLY AKUBALI MZIKI WA YANGA

KOCHA WA AL AHLY AKUBALI MZIKI WA YANGA

801
0
SHARE
Martin Jol-Kocha mkuu wa Al Ahly
Martin Jol-Kocha mkuu wa Al Ahly
Martin Jol-Kocha mkuu wa Al Ahly

Kocha mkuu wa timu ya Al Ahly ya Misri Martin Jol ameukubali mziki wa Yanga na kutoa pongezi kwa baadhi ya idara za wanajangwani kutokana na kukunwa na kiwango walichokionesha kwenye mchezo wa leo wa klabu bingwa Afrika.

Jol amesema licha ya timu yake kupata sare ya bao 1-1 ugenini, mchezo haukuwa rahisi kwao kutokana na upinzani waliokumbana nao kutoka kwa Yanga.

“Kabla ya mchezo tulijua kabisa Yanga ni timu ngumu lakini tulifanikiwa kufunga goli la kuongoza, kipindi cha pili tukafanikiwa kuuteka mchezo”, anasema mchezaji huyo wa zamani wa Bayern Munich.

“Yanga ni timu nzuri inawachezaji wenye uwezo mkubwa, mpira ulivyoanza tu walifanya shambulizi kali lakini hawakuweza kufunga. Tumeshacheza mchezo wa kwanza hivyo tutajipang kwa ajili ya kushinda mchezo wa marudiano bila kuruhusu kufungwa goli”.

“Safu ya ulinzi ya Yanga pamoja na washambuliaji wao wamecheza vizuri kwasababu mabeki wao waliweza kuokoa mashambulizi kadhaa tuliyofanya lakini washambuliaji walitupa presha iliyosababisha goli la kujifunga”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here