Home Ligi EPL EPL: Spurs vs Man Utd – Rekodi ya matokeo mabaya vs United...

EPL: Spurs vs Man Utd – Rekodi ya matokeo mabaya vs United yataendelea na kuikosesha Spurs ubingwa?

893
0
SHARE

Hapo nyuma kidogo Manchester United walikuwa wakitawala sana Premier League na mechi za aina ya timu kama Tottenham zilikuwa zinachukuliwa kama mechi dhidi ya Stoke, Aston Villa au Hull.  
Uwezekano wa Manchester United kuibuka na ushindi katika mechi hizo ulikuwa ni kama kisichoepukika kama ambavyo Roy Keane alivyoelezea katika kitabu chake cha mwaka 2014, akimkariri Fergie katika mazungumzo ya timu kabla ya mechi.
‘ilikuwa mechi dhidi ya Tottenham nyumbani,’ Keane anaandika. ‘Msiifikirie sana Tottenham, wote tunajua wakoje, wazuri lakini hawatishi lakini wote tunafahamu tutawafunga.”

Kwa miaka mingi ya utawala wa Ferguson, kushinda dhidi ya Spurs kilikuwa kitu cha kawaida.
Katika mechi 40 walizokutana katika mfumo wa Premier League ulioanza 1992 mpaka Ferguson alipostaafu mwaka 2013, United 28, sare 8 na kupoteza mechi 4. Mechi vs Spurs nyumbani au ugenini ilikuwa mechi ya uhakika wa ushindi. 

 Wakati huo msimu ulipokuwa unafikia mwishoni, United wangekuwa wanawania ubingwa, wakati Spurs wakiwa wanapambana kujaribu kupata japo nafasi ya 4 kwa ajili ya Champions League.
Hivi sasa, mambo yamebadilika na wapinzani hawa wanakutana tena leo Jumapili @White Hart Lane, kuna mabadiliko makubwa ukifananisha na miaka 10 iliyopita.

Wakati huu ni klabu ya London ya kaskazini ambayo inahitaji pointi ili iweze kuendeea kuwemo kwenye mbio za ubingwa dhidi ya Leicester City na hatimaye kushinda ubingwa, wakati United wanahitaji kushinda ili kuendelea kuwapa presha Man City katika kugombea nafasi ya 4. United wanafahamu kwamba hii ni moja ya mechi zao muhimu za msimu wao. 

  Kama utaangalia maendeleo ya timu hizi mbili kwenye vipimo, utaona tangu kustaafu kwa Ferguson, Spurs taratibu wameanza kuisogelea United inayoporomoka. 

Tukiangalia msimu huu – Spurs chini ya Mauricio Pochettino – wanacheza kwa kushambulia chini ya msingi wa safu ya ulinzi imara, mashambulizi ya kushtukiza yakichagizwa na mabeki wa pembeni kupanda vizuri zaidi. Mashabiki wa United wanatamani kuona timu ikicheza kama zamani, mpira wa kushambulia kwa kasi. Louis van Gaal na kikosi chake wamekuwa mbadala wa Spurs ya zamani wazuri lakini sio imara kama Keane alivyosema kwenye kitabu chake. 
United msimu huu wamerudi nyuma kucheza mpira wa taratibu, usio na madhara wa kumiliki sana mpira. Uwezekano wa Van Gaal kuendelea kwa msimu wa tatu ndio kitu mashabiki wa United hawataki hata kusikia. 

  Lakini bado pamoja na kutokuwa na msimu mzuri United wanaweza kupata chochote kwenye msimu wao katika siku kadhaa zijazo. 

Ushindi dhidi ya Spurs utawapa mwanya wa kuendelea kuipa Man City presha katika nafasi ya 4, ambao jana wameifunga West Brom 2-1, pia watakuwa wamepata hali ya kujiamini kuelekea mchezo wa FA Cup vs West Ham jumatano ijayo. 

Hata hivyo, inaonekana Spurs wanaweza kupata matokeo dhidi ya United. Kikosi cha LVG kinaonekana kupata taabu kucheza na timu zinazoshambulia kwa kasi na Spurs hiyo ndio staili yao, bila kusahau wachezaji walio kwenye ubora wao viungo Dele Alli na Christian Eriksen, na mshambuliaji hatari mwenye goli 22, Harry Kane. 

  United hawajapoteza mechi katika uwanja wa White Hart Lane katika mechi 14 na hata mechi moja waliyofungwa mwaka 2001 ilikuwa kwa sababu kikosi cha Fergie tayari kilikuwa kimeshashinda ubingwa. Lakini muda haumsubiri mtu yoyote katika soka, na mambo yamebadilika. Spurs sasa wanashindani ubingwa wakati United wakiwa ‘underdogs’.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here