Home Ligi EPL SHABIKI WA ARSENAL AFANYA KUFURU KWENYE HARUSI YAKE

SHABIKI WA ARSENAL AFANYA KUFURU KWENYE HARUSI YAKE

704
0
SHARE

Arsena fan

Ushabiki wa soka umewafanya watu wafanye mambo mengi ambayo yamewashangaza na kuwashtua wengi, kuna ambao wanafikia hata kukatisha maisha yao kwasababu timu zao zinapata matokeo mabaya. Kuna wengine wamefanya vituko ambavyo havielezeki kwasababu ya kuzipenda timu zao na soka pia, sasa kutana na hii….

Shabiki mmoja wa Arsenal huko nchini Malaysia aliamua kufunga ndoa ya gharama kubwa weekend iliyopita wakati The Gunners wakiibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0 dhidi ya Watford ukiwa ni mchezo wa Premier League.

Arsena fan 1

Ehemu ya kucheea musiki ilikuwa imepambwa na kiuwanja kidogo huku sehemu ya kulia chakula ya wawili hao ikipambwa na rangi za klabu ya Arsenal.

Wanandoa hao ambao walikuwa hawajavalia uzi wa Arsenal, walikuwa wamezungukwa na wapambe ambao walivalia jezi ya nyumbani ya wakali hao wa jijini London kwa ajili ya kupata picha za kumbukumbu.

Arsenal fan 2

Arsena iko nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Premier League lakini wakiwa bado na matumaini ya kutwaa ndoo ya EPL huku wakijua fika wanahitajikufanya kazi ya ziada kuiangusha Leicester City inayoongoza ligi pamoja na Spurs walio nafasi ya pili.

Arsenal fan 3

Angalia picha zaidi hapa chini kushuhudia kijana alivyoalivoipamba arusi yake kwa rangi za Arsenal na mambo mengine kibao yanayohusiana na mchezo wa soka.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here