Home Kitaifa SALEH ALLY: KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA  WA RUSHWA TFF NDIYO MAPINDUZI YA SOKA

SALEH ALLY: KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA  WA RUSHWA TFF NDIYO MAPINDUZI YA SOKA

754
0
SHARE
Saleh Ally-Mhariri kiongozi gazeti la Champion
Saleh Ally-Mhariri kiongozi gazeti la Champion
Saleh Ally-Mhariri kiongozi gazeti la Champion

Mhariri kiongozi wa gazeti la michezo la Champion Saleh Ally na mmiliki wa blog ya habari za michezo inayofahamika kwa jina la salehjembe amesisitiza viongozi wa TFF wanaotuhumiwa kwenye kashfa ya upangaji matokeo pamoja na rushwa wafikishwe mahakamani ili ukweli upatikane na sheria kuchukua mkondo wake.

Mwandishi huyo mkongwe na mchambuzi wa masuala ya michezo nchini amesema njia pekee ya kuliokoa soka la Bongo ni kuwafikisha watuhumiwa kwenye mamlaka zinazohusika kwa hatua zaidi.

“Kwanza tukubali kilichotokea ni kitu kibaya, pili tuwe wazi kwamba kusifanyike ‘figisufigisu’ kwa ajili ya kuhifadhi hiki kilichopo. Nimeona mkurugenzi wa mashindano wa TFF maejiuzulu, nimeona msaidizi wa rais wa TFF amesimamishwa kazi sasa kinachotakiwa ni vyombo vya kisheria kuchukua hatua ili tujue na kupata ukweli ambao utakuwa umepatikana kwa njia za kitaalamu kuhusiana na masuala haya”, alimesema Saleh Ally wakati akihojiwa na kituo cha radio cha Clouds FC kupitia kipindi cha Sports Extra.

“Lakini nionye kwasababu nimeona kuna mipango ambayo inafanyika kutaka kuizuia na kuifanya ile ‘clip’ ya sauti kwamba kuna watu waliitengeneza au wale waliokuwa wakizungumza siyo wenyewe. Mimi sidhani kama unaweza tukatumia nguvu nyingi kuizuia ile clip ionekane ni ya uongo utafikiri tunafanya mipango ya kuikuza Serengeti Boys iwe timu bora ya taifa ya baadaye”.

“Kama kuna ujanja utakuwa unafanyika au mipango ya kuzuia hao wanaotuhumiwa kufanya maovu wasifikishwa kwenye vyombo vya sheria na ikiwezekana sheria kuchukua mkondo wake, basi itaonesha kabisa kunaviongozi wengine ndani ya TFF nao wamekuwa wakishiriki hili.”

“Tumekuwa tukilalamika kwamba kwenye mpira kuna rushwa na tumekuwa tukiamini rushwa wanachukua waamuzi au wachezaji sasa tuhuma hizi zimo ndani ya TFF ambaye ndiye baba wa soka la Tanzania”.

“Kama tutaacha hili tatizo liendelee ndani ya TFF naamini mpira wa Tanzania ndiyo utakuwa mwisho wake, lakini kama tutakubali wanaofanya upuuzi wa namna hii wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na sheria ichukue mkondo wake mimi naamini haya ndiyo yatakuwa mapinduzi ya mpira”, aliongeza huku akikumbushia sakata lililowapeleka jela baadhi ya viongozi wa kipindi cha nyuma wa iliyokuwa FAT.

Tangu kuvuja kwa sauti za viongozi wa ngazi za juu TFF wakisika kupanga njama za kupanga matokeo na kuchukua rushwa, wadau wengi wamekuwa wakitaka viongozi hao kufikishwa kwenye mamlaka zinazohusika na masuala hayo kwa ajili ya uchunguzi wa kina.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here