Home Kitaifa KANU: VIJANA NI MTAJI WA MAFANIKIO YA SOKA LA KESHO

KANU: VIJANA NI MTAJI WA MAFANIKIO YA SOKA LA KESHO

656
0
SHARE
Nwankwo Kanu akikabidhiwa zawadi ya jezi ya Tanzania na Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine
Nwankwo Kanu akikabidhiwa zawadi ya jezi ya Tanzania na Katibu Mkuu wa TFF Mwesigwa Selestine katika tafrija fupi iliyomkutanisha Kanu na wadau wa soka

Usiku wa April 8, 2016 Star Times iliwakutanisha wadau wa soka Tanzania na Nwankwo Kanu mkali wa zamani wa Arsenal, Inter Milan, Ajax na timu ya taifa ya Nigeria The Super Eagles kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo ya soka la Tanzania pamoja na Afrika kwa ujumla.

Shaffih Dauda akipiga story na kubadilishana mawazo na Kanu
Shaffih Dauda akipiga story na kubadilishana mawazo na Kanu

Katika hotuba yake fupi aliyoitoa kwenye ukumbi wa Serena Hotel, Kanu amesema mafanikio yoyote ya soka yanaletwa na vijana.

Mwesigwa pia alimpatia Kanu mpira kama zawadi kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
Mwesigwa pia alimpatia Kanu mpira kama zawadi kutoka Shirikisho la soka Tanzania (TFF)

“Watoto wadogo wakiandaliwa katika misingi bora, watakuwa wachezaji bora wa baadaye na kusaidia mataifa yao. Ni vyema kujenga vituo vingi vya kulelea vijana wenye vipaji na kuwatunza ili kuwafanya wawe baora baadaye”.

Eddo Kumwembe pia alikuwepo kwenye tafrija hiyo ya wadau wa soka na Kanu iliyoandaliwa na Star Times Tanzania
Eddo Kumwembe pia alikuwepo kwenye tafrija hiyo ya wadau wa soka na Kanu iliyoandaliwa na Star Times Tanzania

Lakini akasisitiza kwamba, suala la afya ni muhimu katika soka hususan kwa vijana ambao wanatakiwa kulelewa na kutuzwa kimichezo pamoja na kujali afya zao.

Shaffih Dauda, Nwankwo Kanu pamoja na Mkurugenzi wa Stars Times Tanzania Mr. Lee wakijadili jambo wakati wa tafrija hiyo
Shaffih Dauda, Nwankwo Kanu pamoja na Mkurugenzi wa Stars Times Tanzania Mr. Lee wakijadili jambo wakati wa tafrija hiyo

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here