Home Kitaifa NNAUYE: KWANINI TUNAADHIBU MKOA MZIMA KWA KWA UPUUZI WA WACHACHE? (Audio)

NNAUYE: KWANINI TUNAADHIBU MKOA MZIMA KWA KWA UPUUZI WA WACHACHE? (Audio)

549
0
SHARE
Nape Nnauye-Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo
Nape Nnauye-Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo
Nape Nnauye-Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo

Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo Mh. Nape Nnauye amesema ataipitia ripoti ya hukumu iliyotolewa kwa waliokutwa na hatia kwenye sakata la upangaji matokeo kwenye mechi za mwisho za Kundi C ligi daraja la kwanza.

Adhabu iliyotolewa kwa baadhi ya viongo, waamuzi na wachezaji inaonekana inalalamikiwa kuwakwepa wahusika wakuu na kuwaangukia wale baadhi ambao ni kama wametolewa ‘kafara’ ili kulinda maslahi ya watu fulani.

“Nikirudi Dar es Salaam nataka nisome ripoti ya adhabu kwa zile timu ambazo zinasemwa zilipanga matokeo, lakini hazikai timu kupanga matokeo wanakaa viongozi kupanga matokeo, kwahiyo msingi wa mazungumzo unaanza na viongozi, kwanini tunaadhibu timu nzima?, amehoji Mh. Nnauye. ”

“Kuna kila dalili kwamba kuna viongozi walikaa kupanga halafu wakawashawishi wachezaji wa timu walizozipanga, na inawezekana wachezaji hata senti tano hawakupewa, lakini tunauadhibu mkoa mzima kwa upuuzi wa watu wachache, siwatetei lakini nalifikiria kichwani.”

Hukumu iliyotolewa na Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania inapigiwa kelele na wadau wa soka kutokana na namna ilivyoendeshwa kwa haraka bila kushirikisha taasi kadhaa kama TAKUKURU pamoja na jeshi la polisi kwa uchunguzi zaidi kwasababu shauri hilo linahusisha rushwa ndani yake.

Msikilize Mh. Nape Nnauye juu ya adhabu ya upangaji matokeo-ligi daraja la kwanza

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here