Home Kimataifa KAULI YA KANU KULIKOSOA SHIRIKISHO LA SOKA LA NIGERIA NI SOMO KWA...

KAULI YA KANU KULIKOSOA SHIRIKISHO LA SOKA LA NIGERIA NI SOMO KWA TFF

429
0
SHARE

Kanu-Uganda

Nohodha wa zamani wa kikosi cha Super Eagles Nwankwo Kanu amekosoa uongozi wa Shirikisho la mpira wa Miguu Nigeria (NFF) kwa kusema umechangia kwa kiasi kikubwa kwa timu yao ya taifa kushindwa kufuzu mara mbili mfululizo kiucheza fainali za mataifa ya Afrika.

Nigeria ilikula kusago cha bao 1-0 kutoka kwa Misri juma lililopia na kujikuta ikipoteza nafasi ya kushiriki michuano ya Afrika itakayofanyika Gabon mwaka 2017 na kumwacha Kanu akitupa lawama zake zote kwa NFF.

“Kinachoendelea kwenye soka la Nigeria ni kwamba uongozi wa juu haupaswi kuwa kama ulivyo na hiyo inapelekea athari huku chini,” Kanu aliiambia BBC wakati akifanyiwa maohjiano maalum.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Arsenal alikuwa nchinin Uganda kama balozi wa Unicef pamoja na StarTimes akisaidia kusaka vipaji kwa wachezaji wachezaji wa Uganda watakaokwenda kucheza soka kwenye ligi kuu ya China.

Amesema Shirikisho la soka la Nigeria inabidi libadili staili ya uongozi kama wanahitaji kupata mafanikio.

“Kama kichwa hakiko sawa, basi mwili mzima hauwezi kuwa sawa”, alisema Kanu.

Mchezaji huyo aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika mara mbili amesema lilikuwa ni pigo kubwa kwa Nigeria kushindwa kufuzu fainali za Equatorial Guinea mwaka 2015 na kushindwa tena msimu huu.

Kanu pia amezungumzia hali ya kubadili makocha wa timu ya taifa ya Nigeria. Samson Siasia alipewa kibarua cha muda kukinoa kikosi cha The Super Eagles baada ya kujiuzuli kwa Sunday Oliseh.

Pia akaongeza kwamba, ni vyema kocha atakaepewa timu kwa mkataba wa muda mrefu kama mrithi wa Oliseh awe ni mzawa.

“Mwangalie Stephen Keshi, alishinda ubingwa wa mataifa ya Afrika na kuiongoza Nigeria hadi hatua ya 16 bora kwenye michuano ya kombe la dunia mwaka 2014 nchi Brazil.”

Kanu akiwa nchini Uganda, alipata fursa ya kucheza mpira na watoto wa Katanga na kuangalia baadhi ya mechi za kombe la Star Times.

“Niliangalia mchezo wa kombe la Star Times 2016 kati ya KCCA FC dhidi ya FC Villa na kushuhudia vipaji kutoka kwa wachezaji wengi ambao wanatakiwa kwenda kucheza soka la kulipwa”.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here