Home Kimataifa BAADA YA MPANGO WA KUKUTANA NA MABINTI WA OBAMA KUFELI, MESSI AMETUMIA...

BAADA YA MPANGO WA KUKUTANA NA MABINTI WA OBAMA KUFELI, MESSI AMETUMIA NJIA NYINGINE KUWAFURAHISHA

816
0
SHARE

Argentina vs Paraguay

Wakati Messi akiwa Argentina wiki iliyopita, Rais wa Marekani Barack Obama alisema, mabinti zake walitaka kukutana na superstar wa Barcelona Lionel Messi. Hata hivyo wakati Messi na timu yake ya taifa wanaelekea kukipiga dhidi ya Chile, mabinti hao Malia na Sasha hawakuweza kufunga safari kwenda kukutana na Messi.

Wasichana hao walisikitishwa na kitendo cha kushindwa kukutana na Mess, kitu alichofanya Lionel Messi ni kuwatumia warembo hao jezi za Argentina zilizoandikwa majina yao mgongoni huku akiwa amezisaini.

Malia and Sasha

Sasa kilichobaki ni Barack Obama au Lionel Messi kuamua kukutana wakati wa majira ya joto kwenye michuano ya Copa America, lakini mu-Argentina huyo tayari ameingia kwenye kitabu cha rais Obama kutokana na kitendo chake cha kuwatumia jezi mabinti wa Obama.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here