Home Kimataifa El Clasico: Takwimu 9 za Real Madrid na Barcelona kuelekea mchezo wa...

El Clasico: Takwimu 9 za Real Madrid na Barcelona kuelekea mchezo wa leo – Madrid n rekodi mbovu Camp Nou

2752
0
SHARE

Mchezo wa FC Barcelona vs Real Madrid  kwa sasa inaaminika kuwa ndio mchezo mkubwa zaidi katika soka ambapo wachezaji bora duniani huumana dimbani kwa dakika 90.

Kuelekea mchezo wa Jumamosi, nimekuandalia mkusanyiko wa takwimu mbalimbali ambazo unahitaji kuzifahami kuhusiana na mechi hii kubwa.  

1. Katika mechi zote 85 za Clasico zilizofanyika pale Camp Nou, Barca wamefanikiwa kushinda 49, Madrid wameshinda mara 17, na mara 19 matokeo yalikuwa sare.

2. Barça mpaka sasa hawajapoteza mchezo ambao walianza kufunga goli wakati Real Madrid wakipoteza mechi 1 katika mara 24 ambazo walianza kushinda.

3. Katika vikosi vyote viwili vya sasa vya timu zote mbili, Dani Alves amecheza mechi nyingi dhidi ya Madrid (mechi 26), mara 15 kati ya hizo amecheza akiwa na jezi ya Barca.

 4. Andrés Iniesta na Sergio Ramos wote wamecheza mechi zaidi za El Clasico, mechi 21, Lionel Messi anafuatia kwa kucheza mechi 19.

 5. Cristiano Ronaldo ndio mchezaji aliyecheza mechi nyinginza ligi kuliko mchezaji yoyote katika vikosi viwili. Keylor Navas, Ivan Rakitic na Luis Suárez wote wamecheza mechi 28.

6. Ronaldo pia ndio mfungaji bora wa ligi, akiwa na magoli 28 – idadi kubwa kubwa Mchezaji Yoyote katika vikosi viwili.

 7. MSN wanaongoza linapokuja suala la la assist. Suarez ametoa assist 12 wakati Messi na Neymar wakiwa na assist 10 kila mmoja. Ronaldo, Bale na Koke wanafuatia wakiwa na assist 9 kila mmoja kwenye ligi.

 8. Neymar ametengeneza nafasi kuliko mchezaji wa pande yoyote, nafasi 82, akifuatiwa na Messi nafasi 55, Toni Kroos nafasi 46
9. Safu ya ulinzi, Barca imeruhusu magoli 28 na kupigiwa mashuti kati ya 304. Barca wana clean sheet 13 msimu huu wakati Madrid wana 10.
Golikipa wa Madrid Keylor Navas yupo kwenye top 5 ya magolikipa waliokoa michomo mingi msimu huu, michono (18). Adán (22, Betis), Andrés Fernández (21,Granada), Javi Varas (20, Las Palmas) na Guaita (19, Getafe) – Bravo amefanya save mara 10 tu.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here