Home Ligi EPL China Super League wanataka kumpa Zlatan £1,000,000 kwa wiki.

China Super League wanataka kumpa Zlatan £1,000,000 kwa wiki.

901
0
SHARE

Screen Shot 2016-04-01 at 1.43.10 PM

Baada ya msimu huu kuisha kutakua na story kali kuliko matokeo ya mechi kwasababu kuna majina makubwa yatahusika kwenye movement kutoka kwenye club moja kwenye nyingine. Moja kati ya majina hayo ni Zlatan ambae anamaliza muda wa mkataba wake na PSG.

Club za EPL zimeonyesha interest ya kutaka kumsajili mchezaji huyu lakini kuna habari zinasema kwamba Zlatan anataka mshahara wa Pound laki sita kwawiki. Kama ni kweli akifanikiwa kupata mshahara huo basi atakua ni mchezaji anayelipwa pesa nyingi kuliko mchezaji yoyote ndani ya EPL.

Zlatan Ibrahimovic inasemekana kwamba anataka mshahara wa £600,000 kwa wiki ili ajiunge na club ya EPL. Pia hafurahii ishu ya jinsi kodi kubwa wanayokatwa wachezaji wa kigeni kwenye EPL. Pia kuna club za Super League ya China zipo tayari kumlipa Zlatan £1,000,000 kwa wiki kama akijiunga na ligi hiyo japokua hana interest ya kwenda huko. Maswali ni kwamba kwenye umri wa miaka 34 ana thamani hii ambayo inatajwa?

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here