Home Kitaifa AZAM MWENDO MDUNDO, HAKUNA KULALA

AZAM MWENDO MDUNDO, HAKUNA KULALA

833
0
SHARE
Wachezaji wa Azam FC wakifanya mazoezi kwenye uwanja wao wa mazoezi Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam

Wachezaji wa klabu ya Azam FC, wamefanya mazoezi kwenye uwanja wa mazoezi wa Azam Complex asubuhi ya leo, mara baada ya kuilaza Tanzania Prisons kwa mabao 3-1 jana jioni na kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup).

Kiungo Jean Mugiraneza (kulia) tayari amejiunga na kikosi cha Azam akitokea kuitumikia timu yake ya taifa ya Rwanda
Kiungo Jean Mugiraneza (kulia) tayari amejiunga na kikosi cha Azam akitokea kuitumikia timu yake ya taifa ya Rwanda

Baadhi ya wachezaji waliocheza dakika nyingi kwenye mchezo wa jana leo walifanya mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa kocha Mario Marinica, huku wakimalizia na programu ya kurudisha mwili katika hali ya kawaida kwa kuingia ndani ya mapipa ya maji yenye mabarafu.

Erasto Nyoni akimmwagia maji yenye barafu Ramadhani Singano 'Messi' lilipofika zoezi la wachezaji hao kuingia ndani ya mapipa yenye maji yaliyotiwa barafu
Erasto Nyoni akimmwagia maji yenye barafu Ramadhani Singano ‘Messi’ lilipofika zoezi la wachezaji hao kuingia ndani ya mapipa yenye maji yaliyotiwa barafu

Azam FC imeendelea na mazoezi hayo katika kujiweka sawa kwa mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Toto Africans, utaofanyika Jumapili ijayo (Aprili 3) kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Magolikipa wa Azam wakiangalia kwa makini maelekezo kutoka kwa kocha wao
Magolikipa wa Azam wakiangalia kwa makini maelekezo kutoka kwa kocha wao

Chanzo: Official Facebook Page for AzamFC

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here