Home Kitaifa HIVI NDIVYO STARS ILIVYOKUWA NA NAFASI KUBWA YA KUFUZU AFCON 2017 KAMA...

HIVI NDIVYO STARS ILIVYOKUWA NA NAFASI KUBWA YA KUFUZU AFCON 2017 KAMA CHAD ISINGEJITOA

662
0
SHARE

EDWI0220

Na Baraka Mbolembole

Hakika kitendo cha timu ya Taifa ya Chad kujitoa katika harakati za kufuzu kwa fainali za CAN 2017 ni cha kuchukiza sana hasa wakati huu wa karne ya 21. Upande wangu ni kama kila kitu kimekwisha upande wa timu ya Taifa ya Tanzania (Stars) kwa kuwa nafasi pekee iliyokuwa wazi kwa Stars ni kufuzu kama ‘Washindwa watatu bora katika hatua ya makundi.’

Ilikuwa ni lazima Stars iwafunge tena Chad katika mchezo wa Jumatatu hii endapo ingefanyika kama tulivyotaraji watanzania wote. Kulingana na mwenendo wa makundi mengi 12 jinsi ulivyo, Stars ilikuwa na nafasi kubwa ya kufuzu kama washindwa watatu bora katika makundi 12.

Kumbuka fainali za michuano zitafanyika nchini Gabon mapema mwaka ujao na wenyeji hao tarajiwa wanashiriki michezo ya kufuzu lakini wakiwa tayari na tiketi yao mkononi. Wakiwa ni vinara wa kundi la Tisa mbele ya Ivory Coast, Sudan na Sierra Leone kundi hilo halitakuwa na nafasi ya mshindwa wa pili bora hivyo mathalani kundi likiendelea kuongozwa na Gabon na Ivory Coast kumaliza katika nafasi ya pili kama ilivyo sasa, ‘ Tembo’ watafuzu kama washindi wa kundi.

Kundi la Kwanza

Nasema nafasi ya Stars ilikuwa wazi kwa maana katika kundi la kwanza nchi ya Tunisia ndiyo wanashikilia usukani wakiwa na alama 6 sawa na timu za Togo na Liberia. Timu zote zimecheza mechi 3 hivyo mechi zao za nne zingetoa mwelekeo zaidi kujua ni timu gani ingekuwa na nafasi ya kufuzu kama mshindi wa kundi na mshindwa wa kundi. Stars ingefikisha alama 7 kama ingepata ushindi mwingine dhidi ya Chad.

Kundi la Pili

Katika kundi la Pili, DR Congo wanashikilia usukani wakiwa na alama 6, wanafuatiwa na timu za Angola na Afrika ya Kati zenye alama nne-nne kila moja. Madagasca wanashika mkia wa kundi wakiwa na alama mbili tu. Nje ya DR Congo hakuna timu nyingine katika kundi hili ambayo ingeweza kufikisha pointi ambazo Stars ilitaraji kuzikusanya.

Kundi la Tatu

Benin wana alama 8 baada ya kucheza game nne katika kundi la Tatu, Mali wanafuatia wakiwa na alama 7 pia wamecheza mechi nne, Sudan Kusini wana alama 3 wakiwa wamecheza mechi nne, Mali watacheza mchezo wao wa nne dhidi ya Equatorial Guinea wiki hii.

Watafikisha alama kumi na kuongoza ikiwa watapa ushindi. Kundi hili lina nafasi kubwa ya kutoa timu mbili zitakazofuzu kwa CAN 2017 kwa maana ya mshindi na mshindwa bora. Ni katika kundi hili Stars ilipaswa kuchuana nalo kugombea moja ya nafasi 3 za washindwa bora.

Kundi la Nne

Burkina Faso iliwafunga Uganda katika mchezo uliopita na kuongoza kundi la Nne wakiwa na alama 6. Uganda inafuatia ikiwa pia na alama 6 na mchezo wao wa nne jijini Kampala kesho Jumanne dhidi ya Burkina Faso utawarudisha kileleni mwa kundi.

Botswana walipoteza nafasi ya kufuzu kama washindwa bora wa kundi hili baada ya kukubali kufungwa na Shelisheli katika mchezo wa ugenini, baada ya kuwafunga ‘Wangazija’ hao katika mchezo wa marejeano siku ya jana Jumapili wamefikisha alama 6 sawa na Burkina Faso na Uganda lakini Botswana wamecheza game nne. Kundi hili pia linaweza kutoa mshindi na mshindwa bora watakaofuzu kwa safari ya Ga bon.

Kundi la Tano

Guinea Bissau baada ya kuishinda Kenya katika michezo yote miwili imejikita kileleni mwa msimamo wa kundi la Tano ikiwa na alama 7. Congo Brazaville na Zambia zinafuatia zikiwa na alama 6 kila timu na timu zote katika kundi hili zimecheza game nne-nne hivyo kwa namna yoyote Stars ingekuwa na alama 7 sawa na vinara wa kundi hii.

Kati ya makundi yenye nafasi finyu ya kutoa mshindwa bora ni kundi la tano. Stars ilikuwa na nafasi ya kumaliza na alama nyingi zaidi ya timu ya pili itakayo maliza katika kundi hili.

Kundi la Sita

Morocco wanaweza kuwa timu ya pili kufuzu kwa fainali za mwakani baada ya wenyeji Gabon kama wataishinda tena timu namba moja kwa ubora barani Afrika, Cape Verde siku ya Jumanne. Wakiwa na alama 9 baada ya kucheza gemu 3, Morocco wanashikilia uongozi wa kundi la Sita.

Cape Verde ambayo ilifungwa nyumbani wiki iliyopita wanafuatia wakiwa na alama 6. Kila timu katika kundi hili imecheza gemu 3 hivyo uelekeo wa kupata mshindwa bora pia upo kwa kuwa baada ya uwezekano mkubwa wa kundi hili kuwapeleka Morocco na Cape Verde katika CAN 2017.

Timu nyingine katika kundi hili ni Sao Tome yenye pointi 3 na Libya isiyo na alama yoyote. Baada ya Morocco v Cape Verde timu hizo zitakuwa na kazi rahisi ya kuchukua pointi 6 kila moja kutoka kwa Sao Tome na Libya. Mshindwa bora zaidi ambaye Stars isingeweza kuendana naye angetoka katika kundi hili la Sita.

Kundi la Saba

Kundi la 7 ndiyo hili lililovurugwa na Chad, pia imo Stars, Nigeria na Misri.

Kundi la Nane

Ghana imefikisha alama kumi baada ya suluhu dhidi ya Msumbiji ja siku ya Jumapili. Wanaweza kufuzu kama watashinda mchezo wao wa tano mwezi Juni. Mauritius kama wataishinda tena Malawi watafikisha alama 9 hivyo watakuwa na nafasi kubwa ya kufuzu kama washindwa bora wa pili katika kundi. Nafasi ambayo labda ilikuwa ya Stars inaweza kuangukia kwa taifa hili dogo.

Kundi la Tisa

Kundi la Tisa linajumuisha wenyeji wa fainali hizo, Gabon, Ivory Coast, Sudan na Siera Leone.

Kundi la Kumi

Katika kundi la Kumi, Algeria wanaweza kufuzu kabla ya michezo ya mwezi Juni endapo watapata ushindi dhidi ya Ethiopia ugenini kesho Jumanne. Algeria imekusanya alama 9 katika game zake 3, wanafuatiwa kwa mbali na SheliSheli na Ethiopia wenye alama nne kila moja na timu ya mwisho ni Lethoto.

Zaidi ya Algeri katika kundi hili hakuna timu yenye uwezo wa kuipiku Stars endapo Chad wasingejitoa. Mshindwa bora hawezi kutoka katika kundi hili.

Kundi la 11

Senegal nao watafuzu kama wataifunga tena Niger katika mchezo wa Jumanne hii. Wakiwa na alama 9 baada ya kucheza michezo mitatu, Senegal wanaongoza kundi la 11. Timu za Namibia, Burundi na Niger zikifuatia zikiwa na alama tatu-tatu kila timu ikiwa imecheza game 3. Timu gani hapa ingeipiku Stars? Hakuna.

Kundi la 12

Katika kundi la 12 kuna ushindani mkubwa sana, Swazland inaongoza kundi ikiwa na alama 5 sawa na Zimbabwe, Malawi na Guinea zinafuatia zikiwa na pointi 2 kila timu ikiwa imecheza mechi 3. Katika kundi hili pia hakuna timu ya pili ambayo itapata alama zaidi kama zile ambazo ingeweza kuzipata Stars.

Kundi la 13

Cameroon itasafiria hadi Afrika Kusini wiki hii katika mchezo wa marejeano. Ikiwa na alama 7 zinazowafanya kuongoza kundi la mwisho (kundi la 13) Cameroon inawavaa Afrika Kusini wenye pointi mbili tu baada ya kila timu kucheza mechi 3.

Mauritania inashika nafasi ya pili ikiwa na pointi 6 na wanaweza kufikisha 9 ikiwa wataifunga Gambia katika mechi yao ya nne. Kundi hili pia linaweza kutoa mshindwa bora na Stars ingepambana nalo pia.

Baada ya mechi ya kesho kati ya Misri v Nigeria labda nitaweza kurejesha imani ya kuiona Stars katika AFCON, ila sasa nafasi ni kama imepotelea angani…

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here