Home Ligi BUNDESLIGA Udhamini wa Jezi kufikia€1 billion – EPL kiboko, Spain yashuka kimapato

Udhamini wa Jezi kufikia€1 billion – EPL kiboko, Spain yashuka kimapato

855
0
SHARE

Udhamini wa jezi za vilabu katika ligi kubwa sita barani ulaya kwa sasa  una thamani ya 830 million euros na inakaribia kufikia €1 billion ndani ya misimu miwili ijayo, kwa mujibu wa utafiti.

 Kampuni ya data za michezo ya The Repucom sports data firm imesema kwamba udhamini wa jezi za vilabu vya EPL ndio mkubwa zaidi – udhamini wa jezi za vilabu vya EPL umekuwa kutoka 244 million euros ($273 million) msimu uliopita mpaka kufikia  330 million euros ($370 million) msimu wa 2015/16.
Kwa ujumla, dili la mikataba ya jezi nchini England, France, Germany, Italy, Netherlands na Spain – zimetoka kwenye thamani ya 736 million euros ($825 million) msimu uliopita mpaka kufikia 830 million ($930 million) msimu wa 2015/16.

‘Huu ndio ukuaji wa thamani, tunategemea kuona uwekezaji wa udhamini kwenye jezi ukifikia €1 billion euros kufikia msimu wa 2017/18 season,’ alisema Jon Stainer, mkurugenzi mkuu, Repucom UK.
Manchester United walisaini mkataba wenye thamani ya $600 million na Chevrolet mwaka 2012. Barcelona wanaripotiwa kuwa kwenye mazungumzo na Qatar Airways kuongeza mkataba wao kwa dili linalofanana na United.

 Fedha nyingi za udhamini wa jezi za vilabu hivi vya ulaya zinatoka katika nchi ambazo zipo nje ya mipaka ya ulaya. UAE (Falme za kiarabu), zinatumia 163 million euros, na ndio wanaongoza kwa kutumia fedha nyingi kwenye kudhamini. Emirates Airline inawadhamini Real Madrid kwa kiasi kinachokadiriwa $40 million kwa mwaka na Etihad airline nao wanatumia fedha nyingi jina lao kuwepo kifuani mwa jezi za Man City.
Germany ndio nchi inayofuatia kwa makampuni yake kutumia fedha nyingi kwenye udhamini katika ligi kubwa sita – wakitumia 136 million euros wakifuatia kwa kutumia 87 million euros, hasa kampuni za magari.
Kampuni za michezo ya kamari pia wamekuwa wakitumia fedha nyingi, wanatumia 42 million euros. Nafasi ya 11 katika makampuni yanayotumia fedha nyingi kudhamini jezi.
‘Kwa makampuni, udhamini wa jezi unarudisha faida kutokana na thamani ya kujitangaza kwao. Kuibuka kwa makampuni mengi ya kamari napo kunasaidia kuongeza dili za udhamini kwa vilabu.’ Anasema Stainer.

 Makampuni ya usafiri na utalii ndio wamewekeza fedha nyingi zaidi kwenye udhamini wa jezi – wakitumia kiasi cha 199 millon euros msimu wa 2016/16, tofauti kidogo na msimu uliopita walipotumia 209 million euros.
Baada ya English Premier League, Bundesliga ndio wanafuatia kwa kupata udhamini mkubwa – vilabu vyake vikipokea kiasi cha  168 million euros, kutoka 157 million msimu uliopita.
Kwa upande wa Spain, udhamini umeshuka kutoka  113 million euros mpaka 105 msimu huu, kwa mujibu wa Repucom. Udhamini umekuwa kwa upande wa Ligue 1 kutoka  96 million mpaka 103 million.
Serie A wanapata 83 million euros, wakati ligi ya Netherlands’ Eredivisie wameshuka mpaka 41 million.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here