Home Ligi EPL MAN CITY MTUMBWI WENYE MBAO MUHIMU ZILIZOANZA KUOZA, SASA ZINAVUJA

MAN CITY MTUMBWI WENYE MBAO MUHIMU ZILIZOANZA KUOZA, SASA ZINAVUJA

888
0
SHARE
Manchester City's Sergio Aguero celebrates his hat trick during the Barclays Premier League match at the Etihad Stadium, Manchester.

Manchester City's Sergio Aguero celebrates his hat trick during the Barclays Premier League match at the Etihad Stadium, Manchester.

Na David Wambura

Kila nikiwaangalia City kwenye kila game inayopita naendelea kupata picha ya ukubwa wa kazi ya Pep Guardiola akifika klabuni hapo, ni kweli matokeo ya City hivi karibuni hayajasaidiwa na mbinu mgando za Peregrini (conservative & pragmatic approaches) kocha anaeonekana kuamini na kukifia anachokiamini hata kama hakimpi majawabu sahihi

Kabla ya kuongea mbinu za pellegrin (el engeniero) na Louis van Gaal alivyo mu-out muscle kimbinu Jumapili na namna mbinu zake hizo zilivyowahi mnyima matokeo huko nyuma dhidi ya Stoke, Spurs, Liverpool (timu hizi zote zimetumia mbinu ya aina moja dhidi ya City na kupata matokeo) mapungufu yaliyo sehemu ya midfield ya City ambayo Pellegrini ameshindwa kuyarekebisha kwa takribani msimu mzima licha ya kikosi chake kuwa na uwezo wa kumpa option za kuyabadilisha kwa aina ya wachezaji alionao.

Kabala sijagusia mbinu nianze na tatizo la City ambalo kwa kasi limeanza kujidhihirisha wazi (umri), kwamba City kama nimtumbwi mbao zake nyingi muhimu zimeanza kuliwa na nyingne zimeoza kabisa na hilo linapotokea tunajua nini kinafuata unapokua katikati ya maji.

Ukiwaangalia wachezaji kama Yaya Toure ambaye kutokana na sababu tajwa hapojuu uwezo wake wa kusaidia ulinzi kwenye midfield (trackback) ni almost zero lakini mbaya zaidi hata mchango wake kwenye mashambulizi ya timu yake umepungua sana kwa sasa na hivyo kumfanya ashindwe ku offer lolote la maana wakati wa kuzuia na ku-offer kidgo wakati wa kushambulia ukilinganisha na zamani.

Hilo limemfanya si tu kua mzigo mzito kwa timu yake bali mzito na unachoma (gunia la misumali) kiungo anayekosa sifa hizo mbili kama alivyo Yaya kwa kiwango chake cha karibuni, mbao ndefu ilikua inamuhusu muda mrefu, sasa kwa nini bado kila team sheet inayotoka jina lake limo ni swali analopaswa kujibu Pellegrini (hapa naomba nieleweke kidgo) nazungumzia uwezo/form yake kwa sasa.

Si Yaya pekeyake ambaye umri unaonekana kuanza kumsaliti, wachezaji wengi wa City wa kikosi cha kwanza wana umri zaidi ya 32 au wanaelekea 32 na hivyo wengi ushawishi wao (influence) kwenye kuamua matokeo ya mechi za City umepungua, Silva si yule, Sagna na Clichy, Zabaleta na Koralov, Fernandinho japo nae ni miaka 31 namuondoa hapo sababu mapungufu yake yanaongezwa na udhaifu wa Yaya kwenye kusaidia kuzuia tutaona huko mbele.

Demichelis sihitaji hata kumuelezea na Mangala, ni Mangala mchezaji ambaye kila nikimuangalia naona ni ajali inayongoja kutokea (accident in the making) huyu mapungufu yake nimeshayaimba sana, hana sifa za kumfanya kuwa beki bora, ana poor timing, poor positioning, hana utulivu (composure), si mzuri kwenye kuanzisha mashambulizi toka nyuma hivyo pairing yake na Demichelis ni sawa na kidumu cha petrol na kiberiti ni swala la muda tu kabla ya kile ambacho akili ya kawaida inakitegemea (mlipuko).

Ukiangalia kwa umakini list tajwa hapo juu utagundua wengi wanaelekea miaka 32 na zaidi na hivyo jua linaelekea kuzama, na hili ndiyo tatizo linalowakumba City wachezaji wao wengi wenye mchango mkubwa wanazeeka kwa pamoja na hakuna mpango unaoonekana wazi wa kulithishana (succession plan) ukiacha De Bruyne ambae ni long term succesor wa David Silva, bado sijaona nani atakuja kuziba mahala pa Zabaleta, Clichy, Sagna na Petrov, vipi Yaya na Fernadinho ambao wanaelekea the wrong side of their thirties (upande mbaya wa miaka 30) Delph ni mchezaji mzuri lakini tunamuongelea Yaya Toure hapa na Delph hatakaa awe Yaya Toure, Vidal yule wa Juve angeweza kuwa, Matuidi pia wa pale PSG anashawishi kua box to box kama Yaya wa miaka miwili iliyopita hapa ndiyo naona City ya Guardiola itahitaji operation kubwa (major surgery tofauti na watu wengi tunavyofikiri).

Baada ya umri sasa tuje tatizo donda ndugu la kiufundi la Pellegrini, nimewahi kusema mahala City kwa muda mrefu wamekua na tatizo wanapocheza na timu zenye free midfield runners wengi, labda tujikumbushe free mdfield runners ni wachezaji wa aina gani?

FMR ni aina ya wachezaji ambao wakati wa kushambulia mbio zao huanzia katikati ya uwanja (kwenye midfield) kuelekea kwenye lango la mpinzani kwa kasi, timu inaweza kuwa na washambuliaji lakini hawatulii kwenye box muda wote wanatokea pembeni na kuingia katikati kabla ya kuja kwenye box kwa wingi na kwa kasi.

Hii huwa tatizo kwa mabeki wengi wa kati ambao wamezoea kuwa-mark ma-forward bampa to bampa (hili ndiyo limepelekea uvumbuzi wa mbinu ya forward wa uongo/false number 9) kwa style hii mabeki huwa hawajui wamkabe nani wakati wachezaji wengi wanapovamia kwa kwa kasi langoni hapa ndiyo msaada wa viungo wa kati huhitajika.

Aina ya wachezaji husika ni kama MSN jumlisha Iniesta, EPL pale the kops ni mfano mzuri, Firmino, Sturridge Lalana, Coutinho na hata Milner. Spurs wanao Lamela, Eriksen, Dele Alli na hata Harry Kane huwa hasimami sana kwenye box, Stoke wanao Anautovic, Bojan,Shaqiri na Ibrahim Afellay, hawa ni aina ya wachezaji ambao muda wote hukimbia free kutafta maeneo madogo katikati ya defense na midfield kitaalam wanaita (pocket of spaces).

Moja ya kitu ambacho kiungo yeyote wa kati huwa anafundishwa mapema kabisa ni ‘pick up your runners from midfield’ kimbia na wachezaji ambao wanakimbia kutoka kwenye midfield kuelekea golini kwako na kwamba kwa vyovyote vile usiwaache wakimbie free sababu hujui madhara watakayoenda yafanya kwenye box lako (tunakumbuka mbio za Lampard kwenda kwenye box ya mpinzani zilivyokua zinaleta madhara kwa wapinzani) hivyo viungo huwa wanafundishwa hili mapema kuepusha madhara yanayoweza letwa na viungo dizaini ya super Lamps

Sasa shida ya City kila inapokutana na timu yeyote yenye sifa za wachezaji tajwa hapo juu huwa inapata wakati mgumu kwasababu mtu pekee anaefanya kazi ya ku-pick up runners ni Fernnadinho hasa anapokua yeye na Yaya peke yao katikati kama central midfielders, kwasababu Yaya hawezi tena kimbizana na vijana, ndiyo maana hali huwa tete wanapokutana na kina Coutinho na nduguze huwa wanamuelemea Fernandinho, walau hali huwa ahueni wanapokua watatu yaani, Fernando, Fernandinho na Yaya.

Sasa kwanini el engeniero ameendelea kumpanga Fernandinho pekee na Yaya mara nyingi anapokutana na timu yenye free runners wengi badala ya kuwapanga watatu ni swali la Pellegrini kujibu, alifanya hivyo kwa Stoke na Spurs akapigwa nje ndani, Barca ya MSN na CSKA Moscow ya kina Tosic, Ahmed Musa na Seydou Doumbia akapigwa nyumbani na ugenini kwenye UEFA, the kops ndiyo kajifanyia muembe wake wa uani kwa City

Ndiyo maana hata LVG alikua mjanja kwenye mbinu zake Jumapili katika kuhakikisha anafaidika na mapungufu hayo, alimuanzisha Lingard namba 10, huku Mata akipelekwa kulia kwa hiyo tactical change Utd walikua na free runners wa nne, Martial kushoto akiingia ndani, Rashford asiyetulia kwenye box, Lingard katikati namba 10 na Mata kulia akiingia ndani ndiyo maana City walipata wakati mgumu sana hasa dakika 30 za mwanzo kabla ya Fernando hajaingia na kujaribu kutuliza mambo.

Lengo la kumchezesha Lingard namba 10 lilikua ni kujaribu kukishambulia kiungo cha City ambacho kwa dakika zile za mwanzo mkabali alikua Fernandinho pekee ambae hata hivyo hana mbio na flexibilty ya bwana mdgo Lingard lakini pia wakijua kwa kufanya hivyo watakua wengi wakati wa kushambulia dhindi ya central midfiledrs wawili wa City, kwa kufanya hivyo United waliweza fanya kile ambacho timu nyingne tajwa hapo juu zimewahi fanya na kupata matokeo dhid ya City

Kwa misingi hiyo nikiangalia City kwa makini naona Pep hatakuwa na muda mwingi kusheherekea, itabidi amalize honey-moon yake mapema baada ya kufunga ndoa rasmi na the citizens kwani atalazimika kutoa haraka mbao zilizooza kwenye mtumbwi wa City unaovuja kabla ya watu hawajaanza kulilia kukitoa  kichwa chake.

talking tactics (tuongee mbinu)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here