Home Kimataifa GOLDEN STATE WARRIORS YAREJEA BARABARANI, YASHINDA KWA TABU

GOLDEN STATE WARRIORS YAREJEA BARABARANI, YASHINDA KWA TABU

630
0
SHARE

10644093_1543238745972831_63013399_n

Warriors mpaka sasa haijapoteza michezo miwili mfululizo hata mara moja. Na inatakiwa washinde michezo mitatu iliyosalia ya ugeniniili kuvunja rekodi ya kupoteza michezo michache katika viwanja vya ugenini inayoshikiliwa na Chicago Bulls ya msimu wa 1995-1996. Warriors kwa sasa wana rekodi ya 31-7 wakiwa viwanja vya ugenini.

Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya San Antonio Spurs ambao uliambatana na kushindwa kabisa kuonyesha ubora wao wa kupata mitupo ya pointi tatu huku ukishuhudia Curry na Thompson kila mmoja akipata pointi tatu 1 pekee, Warriors walirejea na kushinda kiume dhidi ya Minnesota Timberwolves.

Draymond Green ndiye aliyeiongoza Warriors kwa kufunga pointi 24, akadaka rebound 9 na kutoa pasi 6 huku Warriors wakipata ushindi wa vikapu 109-104. Klay Thompson aliongeza pointi 17 huku akipata mitupo yake yote 5 ya pointi tatu na Warriors waliweza kurejea katika ushindi wao ijapokuwa Mchezaji wao bora ameendelea kuwa na siku mbya katika upataji wa mitupo yake.

Stephen Curry ambaye alikosa mitupo 11 kati ya 12 ya pointo 3 dhidi ya San Antonio Spurs, alikosa tena mitupo 11 kati ya 17 ikiwemo pia mitupo 7 kati ya 9 ya pointi 3. Hata hivyo alimaliza mchezo na pointi 19, pasi 11 na rebound 7. Warriors sasa ina rekodi ya jumla ya 63-7.

Karl Anthony Towns yeye alifunga pointi 24 na kudaka rebounds 11 huku Ricky Rubio ambaye aliingia NBA katika msimu mmoja na Curry akichukuliwa katika nafasi ya 5 huku Curry akiingia nafasi ya saba alifunga pointi 20 pasi 11 na rebound 4.

Mara ya mwisho timu ya Golden State Warriors kupoteza michezo mara mbili mfululizo ilitokea April 5 na 7 msimu uliopita. Warriors inaendelea kuwakosa wachezaji wake muhimu Andrew Bogut ambaye kafanyiwa vipimo na majibu ya kitabibu yanasubiriwa. Festus Ezili ambaye bado anatibu goti na taaarifa zinasema ameanza mazoezi baada ya kuwa nje kwa majuma sita na pia mchezaji Andre Iguodala.

Warriors ambayo inaongoza kwa michezo minne mbele ya washindani wao San Antonio Spurs wanafukuzia kufikia ama kuvunja rekodi ya Chicago Bulls ya kushinda michezo 72 ya msimu mmoja.

HIGHLIGHTS

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here