Home Kimataifa CLIPPERS YAENDELEA KUTOKUELEWEKA.. YACHAPWA NA NEW ORLEANS PELICANS

CLIPPERS YAENDELEA KUTOKUELEWEKA.. YACHAPWA NA NEW ORLEANS PELICANS

566
0
SHARE

pelicHuku klabu ya New Orleans Pelicans ikiwa inauguza wachezaji wake wanne wa kikosi cha kwanza kwenye vyumba vya upasuaji, mchezaji ambaye naye alikuwa mtu wa majeruhi ya kila mara na mchezaji aliyewahi kushiriki mashindano ya All Star Jrue Holiday ndio kakibidhiwa mikoba ya kuiongoza klabu hiyo.

Jrue Holiday alifunga vikapu 22 na kutoa pasi 8 kwa wenzake katika mchezo dhidi ya Los Angeles Clippers ikiwa ni muda mfupi tu tangu klabu yake itangaze kuwa nyota wa timu hiyo Anthony Davis atakosa msimu mzima uliosalia na kuiongoza klabu yake kushinda 109-105.

Jrue Holiday alisema baada ya mchezo kuwa “kwa sasa naamini kuwa mzigo wote wa kuiongoza timu hii ndani ya uwanja ni wa kwangu mie na nitatakiwa kuubeba”.

Holiday kwa sasa ana wastani wa karibu pointi 17 kwa mchezo na pia akiiongoza timu yake katika ushambuliaji kwa sasa hakuwa peke yake kwani wachezaji kadhaa waliongeza kiwango stahiki katika mchezo huu. Omer Asik alifunga pointi 15 huku pia akidaka rebound 14, Dante Cunningham aliongeza pointi 19 ambazo ni nyingi kwake msimu huu.

Tim Frazier ambaye ni mchezaji wa akiba yeye alifunga pointi 17.  Luke Babbitt aliongeza pointi 14 huku mchezaji mwingine Toney Douglas akifunga pointi 15 kiwango kilichopelekea kocha Alvin Gentry kukiri kuwa ameshangazwa na kiwango cha vijana hawa.

Chris Paul alifunga pointi 24 na kutoa pasi 13 huku mchezaji  J.J. Redick  naye akiongeza pointi 24.

HIGHLIGHTS

 

 

 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here