Home Kimataifa Ajali ya hatari kwenye mbio za Formula 1

Ajali ya hatari kwenye mbio za Formula 1

731
0
SHARE

1

Fikiria pale upo kwenye speed ya 200 M per hour harafu unataka kukata kona na ajali inatokea. Hicho kitu kimetokea kwenye mbio za Formula 1 za kwanza kwa msimu huu zilizofanyoka huko Melbourne.

Dereva Fernando Alonso alifika kwenye kona akiwa na speed ya 200mph akijaribu kumpita Estaban Gutierrez lakini akamgonga kwenye taili moja na kusababisha crash kubwa.

Hatua ya kwanza gari la Alonso liligonga tairi la gari la Gutierrez, hatua ya pili gari la Alonso lilitoka nje barabara, hatua ya tatu gari la Alonso lilizunguka juu chini. Hatua ya nne liligonga chini na kwenda kugonga pembeni.

Ajali hiyo mbaya lakini haikuweza kuchukua maisha ya madereva hao wawili. Walitoka wakiwa wazima licha ya magari yao kuharibika hasa la Alonso.

Gari la Alonso na magari mengine yote ya F1 yana kitu kinaitwa Monocoque ambacho kinamzunguka dereva. Kibox hicho kinatengenezwa na material ya Carbon Fibre ambapo hata gari likipata ajali sio rahisi kuvunjika au kukunjika na kumsababishia tatizo dereva.

2

Baada ya racing Rico Rosberg alishinda mbio hizo akifuatiwa na Lewis Hamilton.


3 4

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here