Home Ligi EPL PELLEGRINI NA KIVULI CHAKE, VAN GAAL NA DAFTARI LAKE PATAMU SANA HAPA

PELLEGRINI NA KIVULI CHAKE, VAN GAAL NA DAFTARI LAKE PATAMU SANA HAPA

565
0
SHARE

Van Gaal vs Pellegrini

Na Gascoigne Brian

Hawa ndiyo makocha wenye presha kubwa kuliko makocha wenzao hasa wale wa nafasi 6 za juu, wote hawa wanajaribu kuishi kwa matumaini.

Bahati mbaya sana daktari wao pia ni mmoja na anatokea sehemu moja. Moja kati ya mahali ambapo pailikuwa sio salama kwenda kwa kipindi hiki hasa ligi zikiwa zimebaki karibu mechi 8 kumalizika basi palikuwa ni Etihad ila kwasasa siyo mahala penye hatari zaidi, kwakuwa nae anaishi kwa matumaini hata Mansour Bin Zayed analijua hili.

Wakati mwingine ubora wa De Gea na utamu wa Martial ndiyo umefanya simu ya Jorge Mendes wakala wa Jose Mourinho kuchelewa kufanya kazi Old Trafford.

Naisubiri sana hii mechi itakayokuwa na ubora wa aina yake ingawa imekuja kipindi ambacho timu zote mbili zinaishi kwa matumaini. Utamu wa mechi hii inategemea na ubora wa Kun Aguero na utulivu wa Mangala na ubunifu wa David Silva.

Bado najaribu kumtazama Pellegrini kivuli chake kinavyozidi kumtafuna huku Van Gaal naye muda mwingi akiwa na daftari lake akiendelea kuandika.

Wakati utakapofika tutajua tu aliye bora na anaestahili kupata matokeo katika mchezo wa leo, huyu mmoja akitegemea sana
ubora wa De Gea huyu mwingine akitegemea utimamu wa Yaya Toure.

Najua unawaza sana ubora wa Kun Aguro ila huyu kiumbe inategemea sana na ubunifu wa Silva utakuwa juu kiasi gani, najua akili ya Man City moja kwa moja wanaiwaza sana PSG kuliko mahasimu wao kutokana na nafasi waliyokuwepo katika ligi yetu.

Mechi inakuja kipindi muhimu ila itakosa utamu muhimu kutokana na nafasi zao kama nilivyosema hapo juu.

Nasubiri sana kuona daftari la Van Gaal na kivuli cha Pellegrini kwa wakati mmoja, najua ntajifunza mengi sana kupitia wao. Usiuwaze sana ubora wa Wenger kwa kipindi hiki maana ndiyo muda wake wa kuwanyamazisha mashabiki wake mdomo, anajua sana kucheza na akili za mashabiki wake katika kipindi hiki.

Najua muda ubora haudanganyi ndiyo maana wengine wapo pale walipo na wengine wanajaribu kutuaminisha kuwa wanaweza fika pale kwa ubora wa vikosi vyao.

Huyu wa Etihad katika game tano za mwisho za ligi kuu nchini Uingereza ameshinda game 1, droo 1 na amefungwa 3 ni udhaifu wa kiasi gani hasa timu kama Manchester City, huyu mwingine nae katika game tano za ligi kuu nchini Uingereza ameshinda 2, droo 1 na amefungwa 2.

Kwangu mimi mechi ya leo bado inasimama kama mechi kubwa ila inakutanisha watu wenye ugonjwa mmoja ambao inategemeana na unafuu wa mmoja wapo kuweza kupata matokeo katika mchezo wa leo.

Wakati mwingine pesa siyo kila kitu katika dunia ya soka ndio maana timu kama Leichester City timu yenye kikosi kisichozidi thamani ya paund million 70 kikikaa kileleni huku vikosi vya Manchester City na Manchester United vikiwa na thamani ya zaidi ya paund millioni 350 hapa ndiyo unakuja kuamini kuwa pesa si kila kitu katika dunia ya soka.

Hata mwanaharakati Alvin Ailey analijua hili kwani aliwahi kusema MONEY IS NEVER-ENDING PROBLEM (PESA HAIWEZI KUMALIZA MATATIZO).

Kaka yangu Eddo Kumwembe anatuambia pesa inasawazisha mlima Kilimanjaro na kuwa kweupe kabisa, ila hata yeye anajua kuwa pesa sio kila kitu katika dunia ya soka.

Wakati dunia ikiendelea kujizungusha katika mhimili wake Pellegrini na Van Gaal wanaendelea kujizungusha katika mihimili yao na kujaribu kutuonesha ubora wao wa wachezaji wao huyu mmoja akiwa na Mata huyu mwingine akiwa na Silva.

Huku Martial akiwa mmoja kati ya wachezaji bora kwa upande wa Manchester United ukimweka kando De Gea, huyu mwingine akiwa na Sterling.

Huyu mbele akiwa na Rashford huyu akiwa na Kun Aguero huyu ndiyo anabaki kuwa staa wa mechi ya leo ambaye pia namuona kama mtu ambaye anaweza akaimaliza mechi kupitia miguu yake.

Naisubiri sana hii mechi niweze pata ninachokiamini kupitia makala hii, maana usawa wa dunia si umeshapatikana katika dunia hii iliyokosa usawa.

PELLEGRINI NA KIVULI CHAKE,VAN GAAL NA DAFTARI LAKE PATAMU SANA HAPA.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here