Home Kitaifa KAMUSOKO-TWITE, TELELA NDANI YA MTU MMOJA

KAMUSOKO-TWITE, TELELA NDANI YA MTU MMOJA

917
0
SHARE
????????????????????????????????????

????????????????????????????????????

Na David Wambura

Kwa kawaida timu inapokuwa bingwa ni ngumu sana kuifanya ikaendeleza makali yake kwa msimu unaofuata achilia mbali ugumu wa kuifanya ikaongeza makali, tumewahi shuhudia kwa Man City huko nyuma na hata Chelsea msimu huu kilichowasibu baada ya kuchukua ubungwa msimu uliopita.

Ila kocha wa Yanga, Van Pujin si tu ameweza ku ‘maintain performance’ ya Yanga msimu huu baada ya kuwa mabingwa msimu ulioisha bali ameweza kuongeza makali yao kwa sajili alizofanya ‘notably’ Donard Ngoma na kiungo Thaban Kamusoko, hiki ni kiashilia cha kocha bora anayejua nini anafanya, aina ya makocha ambao ni ‘meticulous planners’ zingatia mambo muhimu.

Labda nianzie hapa ili nieleweke, Yanga licha ya kuchukua ubingwa last season tuliokua tunaingalia kwa ukaribu tulikua tunajua inamatatizo kwenye midfield na beki wa kati mwenye uwezo unaoshahibiana na ule wa Kevin Yondani moja ya mabeki bora wa kwati nchini.

Kwenye midfield walikuwa njia panda (dilema) hususani kwenye kiungo cha chini, sehemu ambayo mpira wa kisasa umeipa majina mengi defensive midfield, anchor ama deep lying midfield kulingana na ubora na majukumu anayopewa kiungo anayecheza mahala husika.

Yanga walikua na Salum Telela kiungo well skilled, mwenye uwezo mzuri wa kupiga pasi zenye macho, anaefanya mambo rahisi kwa umakini mkubwa lakini hana energy wala physic/strenght ya kutosha.

Upande mwingne wanae Mbuyu Twite ananguvu ana nishati ya kutosha lakini less skilled (hana skills za kutosha) kulinganisha na nafasi yenyewewe.

Hapa ndipo nilipomvulia kofia Pluijm kuja na Kamusoko kiungo ambaye kila nikimuangalia namuona Salumu Telela na Mbuyu Twite ndani ya mtu mmoja, well skilled, uwezo mzuri wa kupiga pasi, anafanya mambo rahisi kwa umakini mkubwa lakini pia ana energy na strenght ya kutosha inayoweza mfanya awe box to box akitaka, na hata kuwa kiungo mchafu kama Himid mao ikibidi hiki ndiyo kinamfanya aweze kucheza nafasi zote za katikati ya uwanja.

Yuko vizuri kiasi anaweza cheza namba 6 kwenye anchor role/defensive mid akawa mchafu kama Himid Mao, anaweza cheza pembeni juu kidogo ya namba 6 lakini bado anaweza cheza kama CAM central attacking midfielder akafika sana kwenye box na kufunga kama ambavyo tumemshuhudia game kadhaa.

Umuhimu wa Kamusoko ndani ya Yanga umekuwa mkubwa kiasi huwezi kuifikiria Yanga bila jina la Kamusoko kukuijia kichwani kwanza, ni kama alivyowahi nukuliwa kocha nguli Vicente Delbosque siku ya kumuaga Xavi Hernandez (kwenye Xavi Hernandez testimonial) kwamba “kuna wakati Xavi alikua vital cog kwenye mfumo wa tik taka  wa Spain kiasi alikua muhimu kwa Spain kuliko hata kocha”.

Nikifikiria ukweli kwamba Spain na Barca walilazimika kufikiria mara mbili style yao na hata kulazimika kubadili kwa kiasi fulani namna wanavyocheza baada huyu midfield general kustaafu nalazimika kukubaliana na Vicente Delbosque, sasa Barca na Spain wamebadilikaje ni maada ya siku nyingne, leo ni Kamusoko.

Kiungo cha timu yoyote ili kiwe bora lazima kiwe na vitu vitatu, strength(steel) nguvu, energy(drive/industry/dynamism) nishati, lakini kubwa zaidi vision(maono).

Katika individual level kiungo bora zaidi wa kisasa ni yule mwenye uwezo wa ku control tempo ya mchezo, hiki ndicho kilichowafanya viungo kama Xavi, Scholes, Pirlo, Alonso, Bastian n.k katika ubora wao waheshimike sana wali-set standard very high kiasi walijiweka kwenye blacket ya pekeyao sababu walikua na uwezo wa kuamua sio tu timu zao bali hata za wapinzani wao wacheze katika tempo/ speed wanayotaka wao.

Kiungo mwenye uwezo wa ku-control tempo ya mchezo lazima awe na sifa kadhaa, composure(utulivu), close control, timing ya wakati gani afiche mpira, wakati gani atoe pasi wakati gani a-turn wakati gani a-dribble, lakini kubwa zaidi machaguo bora ya upigaji pasi (pass selection).

Kiungo bora kabla hajapokea mpira tayari anajua maeno manne anayoweza kupeleka mpira lakini kwanini aamue kukupigia wewe si yule, kwanini apige hapa si kule, muda gani apige pasi kwa kipa, muda gani apige side way, muda gani apige pasi kwenda mbele, muda gani apige cross field, muda gani apige long range kwenda kwenye wing namna anavyofanya chaguo sahihi kati ya hayo machaguo mengi aliyonayo ndiyo inamtofautisha kiungo mzuri na bora.

Wakati naangalia game ya Yanga na APR niliona kitu kwa Kamusoko kilichokua kinafanana na nilichokisema hapo juu, achana na goli kali la Juma Abdul achana na Niyonzima alieonekana usiku kabla ya mechi alilala akimuota Zidane ama akiangalia clip za babu upara, nina sababau za kuamini ushindi ule kwa kiasi kikubwa ulichngiwa na watu wawili kocha Van Pluijm kwenye dugout na Kamusoko ndani ya uwanja.

Kocha sababu Yanga walionekana wanacheza kwa malengo na wanamaanisha (playing with purpose & conviction) kimbinu pia walionekana wanajua nini wanafanya walikua very astute. ungeweza kuona badala ya kurudi nyuma na kukabia karibu na goli lao na ku-invite pressure golini kwao Yanga walionekana wanakabia kwenye final third yao na katikati ya uwanja na hivyo kuliweka goli lao mbali na maforward wa timu pinzani na hivyo kupinguza uwezekano wa kushambuliwa kirahisi.

Lakn pia ungeweza kuona walikuwa wanapiga pasi ndefundefu za chini kwenye defensive zone yao Juma Abdul, Mwinyi Haji wakitanua mbali pembeni.

Bosou na Yondani  pia waki-spilt katikati na kuachiana nafasi kubwa kila walipokuwa na mpira na hivyo kupunguza uwezekano wa APR kufika kwenye mpira na kuweka pressure kirahisi tofauti na kama wangecheza pasi fupifupi ingekua rahsi kwa APR kugombea mipira na kuipata kirahisi.

Mwisho ni namna Kamusoko alivyokua anaamua Yanga na APR wacheze kwa speed/tempo ipi. Ungeweza kuona kila alipokuwa anapokea mpira hakuwa na papara ya kupiga pasi mara zote alikua anachelewa kutoa pasi kitu kilichokua kinawavuta wachezaj wa APR wajaribu kumvamia wakiamini watamnyang’anya mpira.

Kamusoko alikua mjanja na timing yake ilikua nzuri alisubiri mpaka wamemkaribia sana kabla ya kuachia mpira, hili lilisaidia sana  kuwapunguzia pressure wachezaji wenzake na kuwapa option nyingi uwanjani.

Wachezaji wawili au watatu wa timu pinzani wanapokuja kukuvamia kwa pamoja halafu wakaukosa mpira maanayake ni kwamba, wachezaji watatu wa timu pinzani hawako kwenye maeneo yao wako out of position kwasababu wote walivutika kwa kumfuata mtu mmoja na kuukosa mpira kwa pamoja.

Xavi na Scholes walikua bora sana kwenye hili enzi za ubora wao (timing), lakini pia Kamusoko alivutia sana kwa namna alivyokua anachagua muda gani apige pasi kwa Yondani, muda gani apige kwa Barthez, muda gani a-turn apige kwa Niyonzima, muda gani a-dribble asogee kwa Ngoma na Tambwe na lango la mpinzani.

Kwa ninachokiona kwa Kamusoko sasa, football brain na tactical awareness anayoioneesha uwanjani nakiri huyu ni kiungo bora kabisa wa nafasi yake kwa miaka ya karibuni toka Chuji aachie ufalme wake.

Kuelekea mechi ya marudiano nategemea watu hao wawili wawe na big say kwa mara nyingne kwenye matokeo ya Yanga, though nategemea Yanga kwasababu wako nyumbani wacheze mpira wao wa kawaida chini ya Van Pluijm kwenye 4-3-3, expansive football wakicheza kwa nafasi, tempo ya juu tofauti kidgo na walivyocheza ugenini ambapo walionekana ku adopt a more measured, control approach.

Nategemea kuona wakiwa more elusive & effective watumie nafasi, waongeze umakini na wapunguze makosa na kwamba itakua makosa makubwa kuamini mechi ilishaisha Kigali.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here