Home Dauda TV AUBAMEYANG AZIDI KUWA TISHIO ULAYA (Video)

AUBAMEYANG AZIDI KUWA TISHIO ULAYA (Video)

665
0
SHARE

Aubameyang

Tottenham Hotspur wameshindwa kabisa kufurukuta mbele ya Borussia Dortmund na kujikuta wakichapwa kwenye uwanja wao wa nyumbani na kuwaacha wajerumani hao wakitinga robo fainali ya michuano ya Europa League.

Wakiwa walichatandikwa 3-0 kwenye mechi ya kwanza ugenini, Spurs walihitaji kufunga magoli matano ili kusonga mbele baada ya Pierre-Emerick Aubameyang kupiga bao la kwanza kwenye mechi ya jana usiku.

Striker huyo Gabon alipachika tena bao la pili kufuatia shambulio la kushtukiza na kuzima kabisa Spurs ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani.

Son Heung alifunga bao pekee la Spurs lakini timu yake ilijikuta inayaaga mashindano na kushindwa kufuzu kwa hatua ya nane bora kwa mwaka wa tatu mfululizo.

Aubameyang andelea kuwa mwiba Ulaya

Aubameyang amekuwa moja kati ya ma-forward hatari kwenye soka la Ulaya, huku kukiwa na taarifa kutoka vilabu vya Barcelona, Paris St-Germain na Manchester United kutaka huduma ya nyota huyo mwenye miaka 26

Aliendelea kudhihirisha ubora wake baada ya kutupia kambani bao mbili kwenye uwanja wa White Hart Lane akifikisha jumla ya magoli 35 kwenye mashindano yote msimu huu.

Takwimu na rekodi mbalimbali

  • Spurs imefunga magoli kwenye mechi 19 mfululizo kwenye uwanja wake wakatika michuano ya Europa League (jumla ya magoli 49)
  • Son Heung-min ameisaidia Spurs kupata magoli saba kwenye mechi za Europa League msimu huu (amefunga magoli 3, na ku-assist 4)
  • Pierre-Emerick Aubameyang amefunga magoli saba kwenye mechi nane za Europa msimu huu
  • Aubameyang amehusika moja kwa moja kwenye magoli 43 (amefunga magoli 35, na ku-assist 8) kwenye michezo 40 ya Borussia Dortmund kwenye mashindano yote msimu huu
  • Borussia Dortmund amefuzu kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya kwa mara ya tatu ndani ya misimu minne, ilifika fainali ya Champions League msimu wa 2012-13 na ikafika robo fainali msimu wa 2013-14

Angalia magoli yote ya mechi ya Tottenham vs Borussia Dortmund 

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here