Home Kitaifa HAYA NDIYO MATUMAINI YA VAN PLUIJM KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA APR

HAYA NDIYO MATUMAINI YA VAN PLUIJM KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA APR

468
0
SHARE
Hans van der Pluijm-kocha mkuu Yanga SC
Hans van der Pluijm-kocha mkuu Yanga SC
Hans van der Pluijm-kocha mkuu Yanga SC

Kocha mkuu wa timu ya Yanga Hans van Pluijm leo amezungumza na waandishi wa habari kuelekea mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya APR FC ya Rwanda ukiwa ni mchezo wa marudiano baada ya Yanga kupta ushindi wa bao 2-1 jijini Kigali, Rwanda.

Pluijm amezungumza mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na imani yake ya kufuzu kwenda hatua inayofuata ya michuano ya klabu bingwa Afrika, kukosekana kwa Juma Abdul na hali za wagonjwa Said Makapu pamoja na Matheo Anthony.

Juma Abdul ataukosa mchezo wa marudiano dhidi ya APR kutokana na kuoneshwa kadi mbili za njano kwenye michezo miwili mfululizo, lakini kama mchezaji mmoja au wawili wanakosekana unawaleta wachezaji wengine kuziba nafasi. Unawapa hali ya kujiamini na kitu kizuri ni kwamba tumeanza mazoezi mapema Jumanne tangu tuliporejea.

Said Makapu na Matheo Anthony wao wanasumbuliwa na Malaria lakini hadi kufikia Jumamosi tunaamini watakuwa wamepona.

Tutacheza kwa kushambulia pale itakapobidi na tutajilinda tutakapotakiwa kufanya hivyo kwenye mchezo wetu wa Jumamosi. Kwenye michuano hii hasa hatua za kutafuta kufuzu kwenda hatua zinazofuata unatakiwa kushambulia sana.

Kama tutacheza kwa kujituma na kujiamini ninauhakika tutapata matokeo mazuri kwasababu tayari tumeshaonesha kwenye mchezo wa ugenini, vilevile siyo lazima kushinda mchezo wa nyumbani lakini tumejiandaa kisaikolojia na ninaamini tutafanikiwa siku ya Jumamosi na kusonga mbele.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here