Home Kitaifa ‘MA-NAHODHA WATANO’, HANS ANABEBWA NA MASTAA WAKE VIONGOZI NDANI YA UWANJA

‘MA-NAHODHA WATANO’, HANS ANABEBWA NA MASTAA WAKE VIONGOZI NDANI YA UWANJA

839
0
SHARE
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm na Niyonzima wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Friends Rangers
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm na Niyonzima wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Friends Rangers
Kocha wa Yanga Hans van Pluijm na Niyonzima wakielekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo wakati wa mchezo kati ya Yanga dhidi ya Friends Rangers

Na Baraka Mbolembole

MIAKA 9 mfululizo kama mchezaji wa timu ya Taifa ya Rwanda ‘Ammavubi,’ kiungo mchezesha timu Haruna Niyonzima tayari ameiwakilisha nchi yake mara 69 katika michezo inayotambuliwa na FIFA, pia amefanikiwa kuifungia magoli matano.

Niyonzima, 26 alijiunga na Yanga SC katikati ya mwaka 2011, na baada ya kuanza vibaya katika ligi kuu ya Tanzania bara msimu wa 2011/12, kiungo huyo alisaidia sana kampeni za Yanga kushinda ubingwa wake wa 23 msimu wa 2012/13.

Niyonzima yuko katika msimu wake wa tano sasa klabuni Yanga na tayari ameshinda mataji mawili ya VPL (2012/13 na 2014/15) na moja la klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup Julai, 2012) Ni mchezaji wa tatu wa kigeni aliyedumu klabu moja kwa muda mrefu nyuma ya Waivory Coast, Kipre Tchetche na Kipre Bolou wa Azam FC ambao walijiunga na timu hiyo Disemba, 2010.

Niyonzima alianza soka la ushindani mwaka 2005 katika klabu ya Etincelles akiwa na miaka 16, akasajiliwa na Rayon Sports. Baada ya msimu mmoja Rayon, Niyonzima akasajiliwa na timu ya jeshi la Rwanda, APR mwaka 2007 akiwa U19. Ni mwaka huo (2007) aliitwa timu ya taifa ambayo sasa ndiye nahodha wa kikosi hicho.

Alicheza APR kwa misimu minne kabla ya kuondoka Rwanda na kuamua kujiunga na Yanga aliko hadi sasa. Niyonzima alikuwa nahodha wa kikosi cha Yanga kilichoshinda 2-1 katika uwanja wa Amahoro, Kigali, dhidi ya APR katika mchezo wa kwanza wa mzungo wa pili wa ligi ya mabingwa Afrika.

Kocha, Hans Van der Pluijm amekuwa akiwatumia Kelvin Yondan, Niyonzima, Mbuyu Twite au Vicent Bossou kama manahodha wa kikosi chake ikiwa nahodha Nadir Haroub hayupo uwanjani na mambo yameendelea kwenda vizuri.

Hans amekuwa na faida kubwa kwa maana timu yake huwa na viongozi wengi uwanjani. Bossou, 30 amechezea klabu 6 kabla ya kusajiliwa Yanga katikati ya mwaka uliopita. Mlinzi huyo wa kati mwenye nguvu amewahi kuwa nahodha wa timu yake ya Taifa ya Togo ambayo ameichezea mara 25 tangu mwaka 2010 alipoitwa kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 24.

Kelvn, 31 yeye amecheza klabu mbili tu tangu mwaka 2006 aliposajiliwa na Simba akitokea shule ya sekondari ya Makongo. Alicheza Simba hadi katikati ya mwaka 2012 na kushinda mataji matatu ya VPL. Tangu aliposajiliwa Yanga, mlinzi huyo wa kati ameshinda mataji mawili ya VPL katika misimu minne iliyopita.

Kelvin amekuwa sehemu ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania tangu mwaka 2007, kwa maana hiyo naye ana uzoefu mkubwa wa kuwaongoza wenzake uwanjani.

Nadir, 34 ambaye ndiye nahodha wa kikosi cha Yanga tangu kujiuzulu kwa Shadrack Nsajigwa, Mei, 2012 amekuwa mchezaji wa timu ya Taifa ya Tanzania kati ya 2006 hadi mapema mwaka huu alipotangaza kujiondoa katika timu hiyo kufuatia kuvuliwa unahodha.

Nadir ndiye mchezaji mwenye umri mkubwa zaidi katika timu ya Yanga, amekuwa muhamasishaji, mchapa kazi,na mtu mwenye nidhamu siku zote. Kuna wakati alikuwa nahodha wa Stars, Zanzibar Heroes na Yanga na aliweza kubeba majukumu yote hayo na kuyatekeleza.

Wachezaji hawa watano ni chachu ya nidhamu ya kimchezo ya Yanga msimu huu. Mbuyu amekuwa nahodha wa Yanga mara kadhaa pia, naye ni mtu-mchapa kazi na kiongozi kwa wenzake.

Amis Tambwe, Donald Ngoma, Thaban Kamusoko ni wachezaji wengine watatu wa kimataifa ambao wanaweza kucheza mechi kama ‘manahodha wasiovaa beji,’ nidhamu ya Saimon Msuva, Deus Kaseke, Pato Ngonyani, Juma Abdul na Mwinyi Hajji ni ya juu na hali hiyo ikiwepo katika timu mwalimu anakuwa na faida nyingi.

Kwanza kunakuwa asilimia nyingi za maelekezo yake kupokelewa vizuri na wachezaji na kuyafanyia kazi, pia anapopoteza uelekeo katika benchi kuna wachezaji wanaweza kujiongoza katika njia mbadala na kuheshimiana. ‘Ma-nahodha watano,’ Hans anabebwa pia na mastaa wake viongozi ndani ya uwanja.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here