Home Ligi EPL DELE ALLI KARIBU CHAKULA CHA JIONI

DELE ALLI KARIBU CHAKULA CHA JIONI

826
0
SHARE

Dele Alli

Na Gascoigne Brian

Wakati mwingine kila nikiangalia mshale wangu wa saa muda unazidi sana kwenda kasi sijui ni wa sekunde au wa dakika ndio unaoanza kufika pale.Kuna siku niliwahi kumwambia rafiki yangu mmoja hivi [IT IZ BETTER 2 FAIL IN ORIGINALITY THAN 2 SUCCEED IN IMMITATION] [NI BORA  KUSHINDWA KWA UHALISIA KULIKO KUSHINDA KWA KUIGA].

Hakunielewa sana ila nikamwambia ukipata nafasi kwa muda mwingine  nitafute nitakuelewesha zaidi. Muda mwingine maisha ya mwanadamu yanahitaji akili ya ziada kuweza kujua kinachostahili na kisicho bora kwa  wakati mmoja,

Ni muda ambao hata kipofu alitamani sana kusoma nakala zangu na kujua kilichobora na kisichostahili ila ni mipango ya MUNGU tu.

Taratibu dunia isiyo na usawa inaanza kuwa na usawa sasa, ndio maana Leichester City wapo juu ya Man United, Man City, Arsenal na Chelsea ndio usawa unaanza kuja. Kwanini usiwe juu wakati una Mahrez kulia alafu mbele yupo Vardy katikati una Kante na Drinkingwater nyuma una Huth na Morgan alafu kweny benchi la ufundi yupo Claudio ranieri moja kati ya makocha bora kabisa.

Hata Qoquelin ilibidi atolewe sana kwa mkopo ili akomazwe mapema na kuja kuwa mhimili mkubwa wa timu, ndiyo kitu kilichokuja kutokea na kuja kuwa nguzo ya timu. Hata sisi Tanzania ili tufike pale tukubali kuwaandaa watoto wa kina Edo Kumwembe, Gascoigne brian, Shaffih Dauda na Alex Lwambano.

Tunaweza pata mwanga na kutambua wapi tunataka elekea ila kama tutaamua kuendelea kuwakomaza wakina Msuva, Ndemla Domayo, Bocco n.k. basi soka letu la kutaka kuja kuwa  walau Zambia tutalisikia tuu hewani.

Kujua ulipojikwaa ni vizuri sana kuliko kujua ulipoanguka. Nilitamani sana kuwa alipo Domayo ila hatufanani uwezo wa miguu yetu yeye amepewa miguu ya ushindi uwanjani mimi nimepewa  macho ya ushindi katika uandishi wa makala.

Dele Alli unanikosha sana hasa napoiona miguu yako ilivyochanua kwa mazoezi, unatupa tunachotaka kupitia miguu yako, kuna siku utatupa kilichobora na kubaki nacho ndani
yetu tatizo unacheza Spurs huwezi zungumzwa sana mpaka pale utakapo kubali kuja katika ufalme wetu wa Big 4.

Mauricio Pochettino ahsante sana kwa zawadi hii najua hauimbwi sana, hausemwi sana ila unaangaliwa sana hasa kwa hiki unachoendelea kutupa.

Taratibu unaingia katika mioyo yetu na kukubali kile unachofanya na kuamini kuwa utamaliza katika nafasi nne za juu, sijui nani atatoka ili akupishe.

Kuwa na miguu miwili hakuna maana kuwa unaweza fika salama mahala unapohitaji kwenda ila hurahisisha safari yako. Hata mwalimu Nyerere muda mwingine maamuzi yake  ndiyo yametufikisha hapa tulipo, itakapo fika wakati wa chakula cha jioni nitakukaribisha Dele Alli tuweze kula pamoja na k-share mambo mengi.

Ilibidi giza  nene litande huku harufu ya asubuhi ikikaribia kuingia, Harry Kane sina shaka sana nawewe tatizo tuu unaishi katika kivuli cha Wayne Rooney katika timu ya taifa ni kazi ngumu sana au uwe na maamuzi nagumu sana ya kumshinda hata Abramovich kwa kuamini kuwa Chelsea atamaliza katika nafasi nne za juu ndiyo mwanadamu pekee anaeamini ivyo.

Kila nikiangalia mshale wangu wa saa naona dakika na sekunde zinazidi kukimbizana tuu, ila vyote lazima vifike pale kwenye 12. Ndiyo navyozidi kuwaona Leichester na Spurs wanavyokimbiza pale juu wote lengo lao ni kufika Champions League, mmeshashtua wengi sana na mtazidi kushtua wengi sana kwa hiki mnachoendelea kutupa.karibuni katika ufalme mpya wa Big 4 ambayo kunauwezekano mkubwa wa baadhi
ya timu kuwapisha.

Muda endelea kwenda kasi ili dunia iweze kuwa na usawa.
DELE ALLI  KARIBU CHAKULA CHA JIONI.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here