Home Kitaifa DAVID MWANTIKA:  SIMBA SC KUWA NA MICHEZO 3 ZAIDI KUNA JAMBO NALIONA,...

DAVID MWANTIKA:  SIMBA SC KUWA NA MICHEZO 3 ZAIDI KUNA JAMBO NALIONA, JITIHADA ZIMENIFANYA NIITWE STARS

741
0
SHARE
David Mwantika-beki wa kati wa Azam FC na Taifa Stars
David Mwantika-beki wa kati wa Azam FC na Taifa Stars
David Mwantika-beki wa kati wa Azam FC na Taifa Stars

Na Baraka Mbolembole

Wakati Jose Mourinho anakaribia kuutema ubingwa wa Ligi kuu ya England msimu wa 2006/07 mbele ya Sir Alex Ferguson alikuwa akilalamikia sana mpangilo wa ratiba za mechi hasa zile za timu yake wakati huo Chelsea na waliokuwa washindani wao wa karibu Manchester United.

Chelsea ilikuwa imeshikilia EPL kwa misimu miwili mfululizo, wakati United ilikuwa ikisaka taji lao la kwanza baada ya misimu mitatu bila EPL. United ilikuwa ikitangulia kucheza (Jumamosi na Chelsea Jumapili, au Chelsea ilikuwa ikicheza jioni na United mchana).

Ilikuwa, Sir Fergie anakwenda kileleni kwa tofauti ya pointi moja mbele ya Chelsea, na Jose alilazimika kushinda baadae ili kuwaengua United kileleni, baadaye akashindwa kabisa na Manchester United ikashinda ubingwa siku ya mwisho wa msimu.

Jumanne hii nimefanya mahojiano na mlinzi wa kati wa timu ya Taifa (Taifa Stars) na klabu ya Azam FC, David Mwantika.

Licha ya kuzungumzia ugumu uliopo katika ligi, na nafasi yake katika timu ya Taifa na klabuni, Mwantika amezungumzia kitendo cha timu yake kuwa na michezo mitatu nyuma dhidi ya viongozi wa ligi kuu bara, timu ya Simba na kusema kwamba ni jambo lisilopendeza katika ligi yeyote ile duniani.

Ungana nami katika mahojiano haya…

www.shaffihdauda.co.tz: Davi, hongera kwa kuitwa tena timu ya taifa?

MWANTIKA: Asante sana, ninafuraha sana. Kuchezea timu ya taifa ni sehemu ya malemgo yangu nilijiwekea, hivyo sehemu ya ndoto yangu ni kama inakwenda kutimia.

www.shaffihdauda.co.tz: Mara ya mwisho uliitwa Stars lini?

MWANTIKA: Wakati ule ambao tulikwenda na Gambia.

www.shaffihdauda.co.tz: Umeitwa tena Stars wakati huu ambao Tanzania ina walinzi wengi wa kati wanaofanya vizuri katika ligi. Nimeona jitihada zako kwa misimu miwili sasa lakini ulitegemea kweli kuitwa Stars wakati huu?

MWANTIKA: Kila mchezaji ana malengo yake, hatakama wachezaji wapo wengi kiasi gani na wanafanya vizuri wakati huu naimani kila mtu ataitwa kikosini kwa muda wake.

Kama muda wangu umefika, Mungu kaniona. Huu ni wakati wangu sasa ni kwenda kufanya kazi nzuri ili kujenga imani yangu zaidi kwa kocha ambaye ameniona na kunijumuhisha katika timu. Nimecheza zaidi ya mechi 15 katika klabu yangu na kujitahidi kufanya kazi yangu vizuri.

www.shaffihdauda.co.tz: Nahodha msaidizi Aggrey Morris amepona majeraha yake na alipangwa kwa mara ya kwanza wakati wa mchezo wa CAF dhidi ya Bidvest Wits siku ambayo ulikaa benchi. Kurejea kwa Aggrey kuna fufua tena ushindani wenu. (walinzi wanne wa kati katika nafasi mbili,  Paschal Wawa, Aggrey, Mwantika na Said Mourad) mimi nauona ushindani wenu umekuwa na maana sana kwa kila mmoja kwa sababu kila mtu anajituma katika mazoezi na hilo limefanya kuwa timamu kimchezo kila inapotokea nafasi kwa mmojawapo, unasemaje kuhusu urejeo wa Aggrey?

MWANTIKA: Kurejea kwa Aggrey kumenifurahisha sana, kwanza kama mchezaji, yeye ni mchezaji mkubwa, ana uzoefu mkubwa pia kwa maana hiyo anakuja kuimarisha zaidi timu. Aggrey amekuwa mshauri wangu, mwalimu wangu, na mara zote amekuwa akinifundisha vitu vya kufanya.

Na uwepo wake kama mshindani wangu wa namba umekuwa sababu ya mimi kuendelea kufanya vizuri. Nina mkaribisha kikosini kwa moyo mkunjufu, yeye ni kiongozi wetu mwingine katika timu.

www.shaffihdauda.co.tz: Mwalimu, Stewart Hall ameonekana kumpa nafasi kila mmoja, wewe, Aggrey, Mourad na Wawa, unazungumziaje utaratibu wake huo?

MWANTIKA: Kocha amekuwa na utaratibu mzuri, kumpa kila mchezaji nafasi ya kucheza ni vizuri ikiwa wachezaji wenyewe kila mmoja hufanya vizuri katika nafasi inayomjia. Stewart amefanya kila mchezaji kuonyesha uwezo wake, na ili kuendelea kumuaminisha mwalimu kila mmoja amekuwa akitumia vizuri nafasi yake.

www.shaffihdauda.co.tz: Unazungumziaje mbio za ubingwa katika ligi kuu kati yenu Azam FC, Yanga na Simba?

MWANTIKA: Ligi bado ni ngumu sana, lakini kuna jambo linaendelea silielewi. Kitendo cha timu moja kuwa nyuma pungufu ya michezo mitatu, hakipo katika ligi yeyote ile hata barani Ulaya.

www.shaffihdauda.co.tz: Ratiba ndiyo imepelekea hali hiyo, kuna siku mnakuwa na mechi za kimataifa hivyo katika ligi hamtacheza, lakini ratiba ya Simba inawaruhusu kucheza, tatizo liko wapi au mnahitaji mechi zao pia zisogezwe mbele, ama pengine matokeo yao yanawapa presha?

MWANTIKA: Hata kama, wanacheza mfululizo mno.

www.shaffihdauda.co.tz: Kwani hali hiyo inaweza kuletea kitu gani?

MWANTIKA: Mechi zetu zinakuwa ngumu zaidi ya kama tungecheza pamoja. Kila timu inakuja kucheza na sisi kwa kutukamaia, mfano, subiri mechi yetu na Stand United (itachezwa leo, Chamanzi Complex.)

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here