Home Kimataifa SAFARI YA DAUDA KUTOKA FIFA HADI GENK KWA SAMATTA (PART II)

SAFARI YA DAUDA KUTOKA FIFA HADI GENK KWA SAMATTA (PART II)

2247
0
SHARE
Shaffih Dauda na Mbwana Samatta wakiwa kwenye mitaa ya jiji la Genk Belgium wakati Dauda alipomtembelea Samatta hivi karibuni
Shaffih Dauda na Mbwana Samatta wakiwa kwenye mitaa ya jiji la Genk Belgium wakati Dauda alipomtembelea Samatta hivi karibuni
Shaffih Dauda na Mbwana Samatta wakiwa kwenye mitaa ya jiji la Genk Belgium wakati Dauda alipomtembelea Samatta hivi karibuni

Safari ya Dauda kutoka FIFA hadi Genk kwa Samatta inaendelea, Part I iliishia pale tayari tumeshafika nyumbani kwa Samatta na tumemlipa dereva tax euro 15, kiasi kikubwa cha pesa ukilinganisha na umbali tuliotumia.

NYUMBANI KWA SAMATTA

Kama ilivyo ada lazima mgeni apokelewe kwa mitindo na mbwembwe bwana. Baada ya kufika kwa Samatta, akatupokea kwa bashasha na kitu cha kwanza anachofanya ni kututembeza katika nyumba anayoishi ambayo ipo ghorofa ya tatu.

Nilichogundua ni kuwa anaishi peke yake katika nyumba hiyo yenye sebule kubwa kwa chini, jiko na sehemu ya kufulia nguo. Juu kuna chumba chake cha kulala kikubwa na kingine kwa ajili ya wageni wake.

Sebuleni kwa Mbwana Samatta mahali ambako hupumzika anapokua amechoka kutokana na shughuli mbalimbali za siku
Sebuleni kwa Mbwana Samatta mahali ambako hupumzika anapokua amechoka kutokana na shughuli mbalimbali za siku

Kama nilivyosema huku na Dar kwa sasa mambo yanatofautiana. Baridi ni kali na kutokana na hali hiyo, hata matumizi ya AC yanatofautiana na Dar kwetu. Hivyo Samatta anaiweka nyumba katika mfumo wa joto kwa kuwasha AC zinazoweka mfumo huo, kidogo tunapata ahueni.

Tunazungumza mambo mbalimbali ya Tanzania na uchaguzi wa Fifa na muda unakwenda, usiku unaingia lakini kwakuwa huwa sisahau ahadi nikamkumbusha kuhusu suala la kupikiwa ugali na samaki. Samatta akacheka sana, akanijibu; “Kaka huku unga tabu kuupata, lakini hakijaharibika kitu twendeni kwenye mgahawa tukale.”

Mbwana Samatta, Shaffih Dauda na Raymond Charles wakipata 'msosi' baada ya Samatta kushindwa kupika ugali samaki kwasababu ya kukosa unga kwenye mji wa Genk, Belgium
Mbwana Samatta, Shaffih Dauda na Raymond Charles wakipata ‘msosi’ baada ya Samatta kushindwa kupika ugali samaki kwasababu ya kukosa unga kwenye mji wa Genk, Belgium

Tukajongea mgahawani kwani hakuna umbali na baadaye tukarejea nyumbani na kupiga stori za hapa na pale.

Acha nioshe macho bila maji, ukutani mwa sebule ya Samatta nagundua kuna televisheni kubwa kama inchi 42 hivi lakini hii ni ‘android tv’, ni ya kisasa iliyounganishwa na mfumo wa internet yenye kasi.

Muda mwingi Samatta hutumia tv hii kutazama mambo mbalimbali ikiwemo video kutoka Youtube, anatazama vipande mbalimbali vya video za Cristiano Ronaldo wa Real Madrid ambaye ni mchezaji anayemvutia. Huyu jamaa ameshasahau kukumbatia laptop akiwa kwenye kochi.

Hii ndiyo tv ya mbwana Samatta, mahali ambapo anatumia muda wake mwingi ukiachana na soka
Hii ndiyo tv ya mbwana Samatta, mahali ambapo anatumia muda wake mwingi ukiachana na soka

Nikamuuliza Samatta huwa anapenda kutazama kitu gani kutoka nyumbani, akanijibu: “Ukiachana na mambo ya habari, napenda sana kutazama vichekesho vya Kingwendu, huyu jamaa namkubali sana.”

Nani asiyelipenda hili jambo hapa ambalo hata yeye Samatta anakiri kuwa inambidi pia kutazama video za MSN wa Barcelona yaani Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar wakifanya vitu vyao uwanjani.

Siku inayofuata yaani Jumapili, kuna mechi ya Ligi Kuu kati ya Genk na Club Brugge, hivyo Samatta anasema ni lazima alale mapema apate muda mwingi wa kupumzika. Ananikumbusha umuhimu wa kuheshimu kazi, nikawaza wachezaji wetu kama hufanya hili, najua hata wewe unayesikiliza umekumbuka majina kadhaa kichwani mwako.

Lakini kabla hajajikaribia kitanda kuvuta shuka, napewa maelekezo kwamba natakiwa kukutana na Mkuu wa Mawasiliano wa Genk, Willem Boogaerts ili tupewe taratibu za kuingia uwanjani katika mchezo huo. Baada ya kuwasiliana naye, Boogaerst anatuelekeza kufika uwanjani saa 7:00 mchana tena twende moja kwa moja katika geti linalotumiwa na waandishi wa habari.

‘NATEMBEA NA MAJINI YA SAMATTA’

Hiyo ilikuwa mechi ya tatu ya Samatta kuichezea Genk akiwa hajafunga hata bao moja, nikiwa na tamaa kama ilivyokuwa kwa watanzania waliowengi kumwona Samatta akiweka kambani, kwa utani nikamweleza; “Kesho utafunga mwanangu.”

Shaffih Dauda na Mbwana Samatta wakiwa kwenye mitaa ya jiji la Genk Belgium wakati Dauda alipomtembelea Samatta hivi karibuni
Shaffih Dauda na Mbwana Samatta wakiwa kwenye mitaa ya jiji la Genk Belgium wakati Dauda alipomtembelea Samatta hivi karibuni

Kwa tababsamu maridadi lilionyesha kuwa hata yeye alingojea hiyo siku kwa hamu akanijibu, inawezekana kwani mara kadhaa umekuwa ukinitamkia vitu na vinatokea kweli, akatania kwa kusema; “Wewe jamaa utakuwa unatembea na majini yangu ujue, yaani ukisema kitu kinatokea kweli.”

Toa pamba masikioni na unaweza kusitisha kidogo unachokifanya usikilize hili jambo dogo kwanini Samatta alinitamkia hivyo. Kauli hiyo ya Samatta, imekuja kwa maana kuna mifano miwili mikubwa iliyo hai ambayo niliwahi kumweleza na ikatokea. Kwanza ni katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Etoile du Sahel, katika mechi ya marudiano jijini Lubumbashi.

Nilimwambia atafunga bao na kuipa ubingwa timu yake, kweli ikatokea hivyo. Pili ni katika tuzo za mwanasoka bora wa Afrika anayecheza Afrika. Kuna kitu kilitokea ambacho wengi hawakufahamu kabla.

Siku chache kabla ya kwenda katika tuzo hizo, nilijua nitaenda na Samatta, hivyo nilijitolea kama Mtanzania mwenye hamasa kushona suti yake ambayo angetwalia tuzo kwani ni heshima na kumbukumbu ambayo ningetaka kuiona kama binadamu mwingine yoyote. Lakini wakati nikiwa katika maandalizi ya safari hiyo kuna jambo lilikuwa likiendelea ambalo sikulifahamu.

Leo nakung’ata sikio kuwa, jambo lenyewe ni kwamba, yule kipa wa TP Mazembe waliyekuwa wakiwania tuzo pamoja na Samatta, yaani Robert Kidiaba alimpigia Thomas Ulimwengu simu na kumueleza, yeye (Kidiaba) amepigiwa simu na watu wa Caf (Shirikisho la Soka Afrika) kwamba mshindi ni yeye.

Simu ya Kidiaba kwa Ulimwengu ilikuwa inalenga ujumbe umfikie Samatta halafu asiende Nigeria katika sherehe za utoaji wa tuzo hizo. Ulimwengu alifikisha ujumbe huo kwa Samatta,  kwa kuonyesha kukata tamaa, kweli Samatta akamueleza basi hakuna haja ya kwenda.

Lakini wenyewe walipokaa na kuchanganua mambo kwa undani, wakaona Samatta inabidi aende kwa maana mimi nilikuwa nimeshaingia gharama ya kushona suti na kuona kuwa ilikuwa Tunu kwake kupata japo nafasi ile huku watu Zaidi ya milioni 40 wa Kitanzania wakimwombea dua njema.

Ndio maafikiano yakafikiwa ingawa kwa shingo iliyopinda kuwa  Samatta aende lakini hakuwa na amani maana tayari Caf ilimtaka Kidiaba ashinde. Kichwa na kinywa cha Samata vilishakubaliana na uongo wa Kidiaba; na hakusita kunambia “Kaka siwezi kushinda, amini hivyo na utaona.”

Kazi yangu kubwa ilikuwa ni kumtia moyo na kumueleza kuwa ni lazima atashinda na ni ngumu sana kwa kipa kupata tuzo hiyo halafu akaachwa mfungaji bora ukizingatia dunia hii ya Messi na Ronaldo ambayo Neuer hapewi stahiki zake.

Maneno yangu sio sheria lakini walau maombi yangu yalijibiwa. Kweli, Samatta akashinda tuzo hiyo na kuitoa kimasomaso Tanzania. Ndiyo maana nikamweleza tena, kwamba atafunga bao katika mchezo huo dhidi ya Brugge.

Samatta-tuzo 1

Ungana nami tena kwenye Part II ujue zaidi nini kiliendelea kwenye safasi hii…

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here