Home Ligi EPL Phra Prommangkalachan: Kiongozi wa kibudhaa aliye nyuma ya mafanikio ya Leicester City

Phra Prommangkalachan: Kiongozi wa kibudhaa aliye nyuma ya mafanikio ya Leicester City

791
0
SHARE

Leicester City kuongoza ligi kuu ya England mpaka kufikia mwezi March ni jambo ambalo limezua gumzo kubwa miongoni mwa wafuatiliaji wa soka duniani. Timu ambayo ilikuwa haipewi nafasi hata ya kubaki ligi kuu kwa msimu mwingine sasa inaelekea kutwaa ubingwa wa EPL.

  Mafanikio ya Leicester yamekuwa yakiwashangaza wengi, lakini sasa imefahamika pamoja na vitu vingine – kuna siri nyuma ya mafanikio haya – kiongozi wa dini ya kibudhaa kutoka Thailand. 

Phra Prommangkalachan, kiongozi wa dini ya kibudhaa, amekuwa akiitembelea mara kwa mara Leicester katika kipindi cha misimu mitatu iliyopita, akija kwa madhumubi ya kuwaombea wachezaji na kuibariki uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo. 

Phra anaamini kwenda kwake mara kwa mara katika klabu hiyo kunaweza kuwa kumechangia kuifanya timu ifanye vizuri – Leicester wapo juu kwa pointi 5 kwenye ligi mbele ya Spurs wanaofuatia nafasi ya pili – huku ikiwa imebaki michezo 8 ligi kumalizika. 

  “Kuna vitu nawapa wachezaji wanavaa shingoni na sina uhakika kama kama wanaelewaga ninachowaambia kuhusiana na vitu hivyo, ila nadhani wanaelewa kwamba madhumuni ni kuwaletea bahati kwejye kazi yao.” –   Phra Prommangkalachan. – aliiambia AFP. 

Vichai Srivaddhanaprabha, mmiliki wa ameripotiwa kuwa muumini mkubwa wa imani hiyo kibudhaa, jambo linaelezewa kwanini aliamua kumleta kiongozi kiongozi wake katika klabu yake.  

  Bwana Phra anaamini kwamba Leicester watafanikiw kutwaa ubingwa mwishoni mwa msimu.. 

  

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here