Home Entertainment IKIWA LEO NI BIRTHDAY YAKE, NDEMLA YEYE HANA HATA MPANGO…

IKIWA LEO NI BIRTHDAY YAKE, NDEMLA YEYE HANA HATA MPANGO…

1925
0
SHARE

IMG-20160315-WA0011

Kuadhimisha siku ya kuzaliwa ‘birthday’ ni jambo muhimu sana kwa kila mtu, mara nyingi sana tumeona watu wakisherekea umbukumbu za siku zao za kuzaliwa.

Weki wamekuwa wakifanya hivyo kwa kufanya part na ku-enjoy na ndugu, jamaa na marafiki kwa kulishana keki na kunywa vinywaji yote katika kufurahi na kuburudika.

Lakini kwa fundi wa mpira pale kwenye klabu ya Msimbazi Simba, Said Hamisi Ndemla mambo ni tofauti kabisa na watu wengine hasa inapofika siku yake ya kuzaliwa.

Leo ni March 15, Said Ndemla anaadhimisha siku yake ya kuzaliwa na anatimiza umri wa miaka kadhaa, shaffihdauda.co.tz imemtafuta Ndemla na kupiganaye story kutaka kujua mambo kadhaa hususan katika siku ya leo ambayo ni muhimu kwake.

Ndemla anasema yeye hana utamaduni wa kufanya tafrija wala sherehe pindi anapoadhimisha siku ya kuzaliwa kwake na huitumia siku hiyo tofauti na watu wengi wanavyodhani.

“Siku kama ya leo (birthday yake) huwa napenda kukaa nyumbani na kumkumbuka baba yangu (mzee Ndemla)”, anasema Ndemla ambaye ni miongoni mwa wachezaji wa Simba walioitwa kwenye timu ya taifa kwa ajili ya mchezo dhidi ya Chad.

“Kitu ambacho huwa napenda kufanya kwenye siku hii ni kwenda kutembelea kwenye kaburi la marehemu baba na kulisafisha tofauti na wengi wanavyodhani labda naweza kufanya sherehe ya kufurahi na marafiki”.

“Lakini pia badala ya kufanya sherehe huwa napenda kufanya dua (kisomo) maalumu kwa ajili yake kwa ajili ya kumuombea kwa Mungu”, anamaliza Ndemla wakati niliyefanya naye mahojiano kwa njia ya simu.

Nilijaribu kumuuliza nyota huyo aliyetokea kwenye timu ya ‘makinda’ ya Simba kwanini amejiwekea utaratibu huo kila inapofika siku yake ya kuzaliwa, nikidhani labda kuna uwezekeno tarehe yake ya kuzaliwa na ya kufariki baba yake zinagongana.

Ndemla amesema hiyo si sababu, ila ni maamuzi yake binafsi kudhimisha siku hiyo kwa namna ambayo amechagua yeye.

shaffihdauda.co.tz inaungana na clab ya club ya Simba, wachezaji, viongozi, wanachama, mashabiki na wadau wote wa soka kukutakia kila kheri katika siku yako ya kuzaliwa.

Happy birthday Said Ndemla 13

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here