Home Dauda TV MAN UTD YATOKEA KWENYE TUNDU LA SINDANO MBELE YA WEST HAM (Video)

MAN UTD YATOKEA KWENYE TUNDU LA SINDANO MBELE YA WEST HAM (Video)

646
0
SHARE

Anthony

Goli la kusawazisha la dakika za lala salama lililofungwa na Anthony Martial kwenye mchezo wa robofainali ya FA Cup limelazimisha mechi ya marudiano baada ya Dimitri Payet kutangulia kuifungia West Ham United kwa mpira wa mpira wa adhabu ndogo uliojaa moja kwa moja wavuni na kuzidi kumpa presha kocha wa United Louis van Gaal.

Payet aliifungia bao West Ham dakika ya 68 akiwa umbali wa mita 30 kutoka golini mpira ambao ulimwacha golikipa wa United David de Gea akiwa hajui la kufanya na kiweka timu yake kwenye mazingira mazuri ya kucheza nusu fainali ya FA Cup.

Baadaye United waliamka baada ya kuingia kwa kiungo mkongwe Bastian Schweinsteiger kuchukua nafasi ya Marouane Fellaini ambapo Martial akabadili matokeo na kulazimisha timu hizo kucheza mchezo wa marudiano utakaoamua nani anasonga mbele kwenye hatua ya nusu fainali.

Angalia video ya magoli yote Manchester United vs West Ham United

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here