Home Kitaifa MBEYA CITY YAAMKIA KWA WAPIGA DEBE WA SHINYANGA

MBEYA CITY YAAMKIA KWA WAPIGA DEBE WA SHINYANGA

693
0
SHARE
Kikosi cha Mbeya City Kilichoanza dhidi ya Simba SC
Kikosi cha Mbeya City Kilichoanza dhidi ya Simba SC
Kikosi cha Mbeya City Kilichoanza dhidi ya Simba SC

Timu ya Mbeya City imeutumia vyema uwanja waken wa nyumbani baada ya kuichapa Stand United ya Shinyanga kwa magoli 2-0 katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliochezwa kwenye dimba la Sokoine, Mbeya.

Ushindi wa Mbeya City umekuja siku chache baada ya kupoteza kwa bao 2-0 mbele ya Simba SC kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa taifa.

Magoli ya Mbeya City yamefungwa na Raphael Daudi ambaye amefunga bao la kwanza dakika ya 12 kwa mkwaju wa penati kufatia mabeki wa Stand United kuunawa mpira kwenye eneo la hatari na mwamuzi wa mchezo huo kuamuru ipigwe penati.

Bao la pili na la ushindi kwa Mbeya City limefungwa na Haruna Shamte dakika mbili baada ya kuanza kwa kipindi cha pili kwa adhabu ndogo baada ya Abdah Juma kufanyiwa madhambi wakati akielekea langoni kwa ‘wapiga debe’ wa mkoani Shinyanga.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here