Home Ligi EPL Liverpool vs Man Utd: Ushindi kwa United Utampa Van Gaal rekodi bora...

Liverpool vs Man Utd: Ushindi kwa United Utampa Van Gaal rekodi bora kuliko kocha yoyote Old Trafford 

741
0
SHARE

Liverpool vs Manchester United: ni moja ya mechi kubwa kabisa katika historia ya soka nchini Uingereza.

 Timu hizi zinakutana kwa mara nyingine tena usiku huu, wakati Jurgen Klopp atakapoiongoza timu yake kupambana na vijana wa Louis van Gaal katika mchezo wa raundi ya 16 bora ya UEFA Europa League.

Wakati LVG akiwa na rekodi nzuri dhidi ya Liverpool tangu alipoanza kuifundisha United – akishinda mechi 4 zote alizokutana nao – lakini vita baina ya vilabu hivi ni kubwa sana na ipo tangu zamani sana.

Mechi ya kwanza kuwakutanisha mahasimu hawa ilikuwa mchezo wa majaribio mnamo mwaka 1894 – miaka miwili baada ya kuundwa kwa Liverpool – na matokeo kwenye mchezo huo Liver walishinda 2-0.

Mechi yao ya kwanza ya ligi ilikuwa mnamo 1895 na Liverpool wakafanikiwa kushinda tena – 7-1 katika ligi ya daraja la pili.


United wakalipiza kisasi wiki 3 baadae walipoifunga Liverpool 5-2.

Kuanzia hapo upinzani ukazaliwa na kuendelea kukua.

Sio tu kwamba timu hizi zipo katika miji ambayo imetengamishwa na umbali maili 35 tu – lakini wote wamekuwa msingi wa maendeleo ya mchezo wa soka nchini Uingereza.

Vilabu hivi viwili ndio vilabu vyenye mafanikio zaidi katika soka nchini Uingereza, wakifanikiwa kutwaa ubingwa EPL mara 38.

Manchester United wametwaa makombe 20 ya ligi na Liverpool wakifanikiwa mara 18.
Hata hivyo, kwenye michuabo ya ulaya, Majogoo wa Jiji ndio wenye mafanikio zaidi kuwazidi Man United.

Liverpool wametwaa makombe 8 mbalimbli ya michuano ya ulaya – yakiwemo matano ya Champions League ukilinganisha na makombe manne kwa United – matatu kati ya hayo yakiwa UCL.

Kwa ujumla Mashetani Wekundu wamefanikiwa zaidi kwa kuchukua jumla ya makombe 62 ukilinganisha na 60 ya upande wa Liverpool.

 Timu zote leo zitaingia uwanjani wakiwa na nia ya kupambana na kuweza kubeba taji la Europa – ndio kombe pekee ambalo wanahesabika kwamba wanaweza kuchukua.
Pia inawezekana kutwaa kombe hili ikawa ndio njia pekee ya kushiriki kwenye UEFA Champions League msimu ujao.

Na Ikiwa United watafanikiwa kushinda leo – Louis van Gaal ataandika historia ya kuwa kocha wa kwanza wa United kuifunga Liverpool mara 5 mfululizo.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here