Home Ligi BUNDESLIGA Kumbe Robert Lewandowski alikua mwizi wa magari..!!

Kumbe Robert Lewandowski alikua mwizi wa magari..!!

735
0
SHARE

lewa2

Kila mtu ana tabia ambayo ameificha au kuna vitu ambavyo alikua anafanya zamani lakini sasa hivi ameacha. Sasa kwa upande wa Robert Lewandowski alikua toto tundu enzi zake akiwa teenager. Kipindi hicho alikua bado yupo kwenye academy ya soka lakini bado alikua mtundu na kucheza michezo ya hatari kama kuiba magari.

Lewandowski amesema hayo yote akiwa kwenye interview na mwandishi wa kitabu chake kipya ambapo jamaa amesema wakati yupo mtoto alikua na makundi ya marafiki ambao waliperekea hadi yeye kuwa mwizi wa magari.

Robert anaendelea kwa kusema kwamba mara nyingine walikua wanaenda kuwarushia polisi maganda ya ndizi au kufanya vitendo ambavyo vitawafanya polisi wajue ni kitu cha hatari na kukimbiza magari yao kuelekea eneo la tukio.

Kwenye moja ya tukio la wizi wa gari akiwa na marafiki zake,Lewandowski anasema mwenye gari alikuja na kisu kama silaha ya kuja kupambana nao baada ya kujua nje kuna wezi wanaiba gari lake.

Kwenye moja ya story akiwa kijana mdogo kwenye academy, Lewandowski anasema aliwai kukamatwa akiwa anavuta sigara kwenye training camp na adhabu yake ilikua ni kuangalia fire extiguisher zote za academy zipo kwenye hali nzuri kwa muda wa miezi 6.

Ukiachana na mambo yake ya wizi wa magari tuangalie kipaji chake cha kusakata kabumbu kupitia Startimes live kwenye Bundesliga.

lewa

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here