Home Kitaifa MATOKEO YOTE YA VPL MECHI ZA MARCH 9, 2016 NA MSIMAMO WA...

MATOKEO YOTE YA VPL MECHI ZA MARCH 9, 2016 NA MSIMAMO WA VPL

747
0
SHARE

Mwadui

Ligi kuu Tanzania bara imeendelea leo kwa michezo minne kuchezwa kwenye viwanja tofauti vya miji ya Tanzania bara.

Mwadui FC ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani Mwadui Complex, Shinyanga imebanwa mbavu na Majimaji ya Songea, Ruvuma kwa kulazimishwa sare ya bila kufungana.

Kagera Sugar ambayo kwa sasa inanolewa na kocha Adolf Rishard imeilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 timu ya wajelajela Tanzania Prisons ya mbeya kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Coastal Union imeweza kujinasua kutoka mkiani mwa ligi baada ya kuinyuka Mgambo JKT kwa bao 1-0 mchezo uliopigwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Baada ya kupata ushindi kwenye mchezo wao uliopita kwenye dimba la Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani, JKT Ruvu imevuna ushindi mwingine leo kwenye uwanja huo kwa kuichapa Toto Africans kwa bao 2-0 na kuendelea kujiweka sawa kwenye msimamo wa ligi

Matokeo yote ya mechi za VPL zilizochezwa leo yapo kama ifuatavyo

Mwadui FC 0-0 Majimaji FC

Tanzania Prisons 1-1 Kagera Sugar

Coastal Union 1-0 Mgambo JKT

JKT Ruvu 2-0 Toto Africans

Msimamo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara baada ya mechi za March 9, 2016 upo kama ifuatavyo

Msimamo

Msimamo 1

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here