Home Kitaifa MAGOLI 39 YA BOCCO, MAGULI, JEREMIAH, AJIB, BADO UNAMLAUMU MKWASA?

MAGOLI 39 YA BOCCO, MAGULI, JEREMIAH, AJIB, BADO UNAMLAUMU MKWASA?

796
0
SHARE
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania Elius Maguli akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza wakati wa mchezo dhidi ya Algeria 

Na Baraka Mbolembole

Washambuliaji wanne kati ya 6 walioitwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wamefunga jumla ya magoli 39 katika ligi kuu ya Tanzania Bara iliyo mzunguko wake wa 21 hivi sasa. Nahodha wa Azam FC, John Bocco alifunga goli lake la nane msimu huu wakati Azam ilipolazimisha sare ya kufungana 2-2 na Yanga SC wikiendi iliyopita.

Elius Maguli tayari amefunga magoli 10, sawa na kijana Ibrahim Ajib wa Simba SC, na mshambulizi anayeongoza kwa ufungaji miongoni mwa wale wazawa, Jeremiah Juma wa Tanzania Prisons tayari amefunga magoli 11.

Wachezaji wote hao wanne wameitwa katika timu ya taifa ambayo itacheza na Chad, Machi 23 katika mchezo wa kugombea nafasi ya kufuzu kwa fainali za CHAN 2017.

NGASSA, LIUZIO, MSUVA NJE

Licha ya kuonyesha kiwango kizuri katika michezo miwili iliyopita ya klabu yake ya Yanga, Saimon Msuva ambaye ni mfunguji bora wa VPL msimu uliopita amejikuta akitemwa kikosi kwa mara ya kwanza ndani ya miezi 18.

Kiungo- mshambulizi, Mrisho Ngassa amekuwa na ‘nafasi ya kuja na kuondoka’ katika klabu yake ya Free State Stars ya Afrika Kusini naye ametemwa kikosini kwa mara ya kwanza baada ya miaka zaidi za 8.

Juma Ndanda Liuzio ni mshambulizi wa kikosi cha kwanza katika klabu yake ya Zesco United ya Zambia, bado hajatulia klabuni kwake kutokana na majeraha ya mara kwa mara ataendelea kuwa nje ya timu ya Taifa baada ya kutemwa katikati ya mwaka uliopita.

Kuachwa kwa washambuliaji hao kumetoa nafasi kwa wafungaji wanaofanya vizuri katika VPL. Nafikiri kocha Charles Mkwassa ameita washambuliaji wazuri.

Ukiwaongeza vijana wengine ‘washindi wa kimataifa,’ nahodha Mbwana Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe bila shaka hatupaswi kuanza kuhoji kuhusu wachezaji walioachwa na badala yake kuwaunga mkono vijana kama Ajib, Maguli na Jeremiah ambao wamefanya jitahada kubwa katika klabu zao.

Mkwassa ameita wachezaji ambao kwa sasa wako fiti kimwili na kiakili, walio katika ubora na utayari wa mchezo ujao. Jeremiah ameitwa kwa mara ya kwanza, uwezo wake wa ufungaji ni wa juu na timu ya Taifa inahitaji wafungaji kama yeye, Maguli, Ajib na Bocco.

Kama watashindwa kufanya vizuri hilo halitamaanisha kuwa Mkwasa amefanya uteuzi mbaya, tutawalaumu wachezaji hao kama watashindwa kufunga magoli katika timu ya Taifa. Kwa sasa Mkwasa yuko sahihi, ameita matarajio ya magoli katika timu yake baada ya wachezaji hao kumshawishi katika michezo ya VPL.

Hajawaitwa ili wasifunge. Amewajumuhisha katika timu ili waendelee kufunga magoli wakiwa Stars kama wanavyofanya katika ligi ya VPL. Kwa ujumla wao (washambuliaji wanne) wamefunga jumla ya magoli 39 katika ligi, si haba ila magoli yao mawili tu dhidi ya Chad yatakuwa na maana kubwa ya uwepo wao katika timu ya Taifa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here