Home Kimataifa Guangzhou Evergrande ya China Super League ina utajiri mkubwa zaidi Manchester United...

Guangzhou Evergrande ya China Super League ina utajiri mkubwa zaidi Manchester United na Real Madrid.

637
0
SHARE

china

China Super League inapata umaarufu mkubwa sana kwa sasa kutokana na usajili wao wa hali ya juu huku wakitoa mishahara ambayo club za Ulaya haziwezi kutoa.

Ripoti imetolewa kuhusu club bingwa ya ligi ya China na kusema kwamba Guangzhou Evergrande ina utajiri mkubwa kuliko club maarufu duniani kama Real Madrid na Manchester United.

Habari hizo zimepewa uzito kutoka kwa kituo cha habari cha China kinaitwa Xinhua kwamba utajiri ambao unatajwa ni mdogo sana ukilinganisha na utajiri halisi wa club hiyo.

Fact ambayo imetumika kuthibitisha utajiri wa club hii ni biashara ambayo wamefanya mwaka jana,Guangzhou Evergrande imefanya biashara yenye thamani ya 3.35 billion dollars. Real Madrid walifanya biashara ya kiasi cha 3.26 billion dollars na Manchester United wakifanya biashara ya kiasi cha 2.35 billion dollars.

Club hii inamilikiwa na kampuni mbili kubwa ambazo zimefanya uwekezaji uliosaidia kukuza jina na soka la Guangzhou Evergrande. Evergrande Real Estate Group wanamiliki 60% na Ali Baba Group inamiliki 40%. Ali Baba ni kampuni ya bilionea Jack Ma mwenye net worth ya US$23.6 billion ambaye ni mfanyabiashara anayemiliki website za Alibaba, Taobab, mifumo ya ulipaji pesa kwenye mtandao kama AliPay na vitu vingine mbalimbali.

Club hii inafanya sana biashara barani Asia kwasababu wameshinda AFC Champions League mwaka 2013 na mwaka 2015. Mashindano haya ni kama UEFA Champions League kwa Ulaya. Wingi wa watu kwa bara la Asia inawapa nafasi ya kufanya biashara kubwa kwasababu ya kuwa maarufu kutokana na ubingwa wa AFC.

Robinho alienda kwenye club hii kufata mapesa na hadi hivi sasa Felipe Scolari yupo hapa akiifundisha club hii. Startimes ndio king’amuzi pekee kinachoonyesha live Chinese Super League, jiunge sasa uone mpira wa pesa.

Comments

comments

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here